Mh. Sebastian Waryuba, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga alifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Katika ziara hiyo, aliweza kukagua ujenzi wa zahanati ya Mpona, kituo cha afya Kipeta, shule shikizi Lyanza na ujenzi wa shule ya sekondari Nankanga.
"Nawaagiza wasimamizi wote wa miradi hii kuhakikisha fidia za ardhi zibalipwa kwa watu wote waliochukuliwa ardhi yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miradi ya
maendeleo" alisema Mh Sebastian Waryuba Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.
pia katika ziara hiyo alifanya kikao ba baraza la ardhi la kata ya Kipeta. "Naomba wakurugenzi wote waliopo katika Wilaya ya Sumbawanga kutoa ;mafunzo na miongozo ya uendeshaji wa mabaraza ya kata ili kuongeza ufanisi wa mabaraza hayo pamoja na kupunguza migogoro inayojitokeza kwenye jamii," alisema Mh. Sebastian Waryuba.
Vile Vile alibahatika kutembelea ofisi za hifadhi ya Uwanda, kisha alishiriki zoezi la kuteketeza zana haramu zinazotumika kwenye uvuvi wa samaki. Baada ya zoezi la uchomaji wa zaha hizo, muhifadhi mkuu wa Uwanda ndugu Orest Njau aliwasii wananchi wanaozunguzka hifadhi hiyo kujiepusha na uvuvi haramu ili kulinda mazalia ya samaki hao.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa