Aliekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg.Missana K. Kwangura leo amekabidhiwa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya wilaya ya Sumbawanga na Ndg. Stephen E Katemba ambae amehamishwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Wakuu wa idara na vitengo Pamoja na watendaji wa kata.
Ndg. Missana Kalela Kwangura ambae kwa sasa ndie Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi lengo kubwa ikiwa kuwahudumia wananchi.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa