Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa ikiongozwa na Hajjat Silafu Jumbe Maufi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa imeridhishwa na ubora wa miradi inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa imefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Imekagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020- 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.
Miradi iliyofikiwa na kamati hiyo ya siasa ni Ujenzi wa madarasa manne Sule ya Sekondari Mazoka, Shule mpya ya Sekodari Kalumbaleza ambayo kwa sasa inatumika, Ujenzi wa madarasa manne Shule mpya ya Sekondari Zimba, Ukaguzi wa ujenzi wa madaraja Muze – Ilemba na kumalizia na ukaguzi wa mradi wa umwagiliaji unaojengwa kata ya Ilemba kijiji cha Ilemba.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa