Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ilianzishwa mwaka 1984 chini ya sheria namba 7 ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inakadiriwa kuwa na eneo la kilomita za mraba 8,871 Kati ya hizo kilomita za mraba 8,203 ni nchi kavu na kilomita za mraba 668 ni eneo la maji.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ina wastani wa Joto kwa mwaka la Nyuzi joto kati ya (24 na 27) kwa kiwango cha juu na kiwango cha chini cha Nyuzi joto (13 na 16). Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ipo Mita 1,700 kutoka usawa wa Bahari. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imepakana na Wilaya mpya ya Kalambo kwa Upande wa Kusini magharibi, Nkasi upande wa Magharibi, Momba upande wa Mashariki na Chunya kwa upande wa Kaskazini.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga makao yake makuu yako Mji mdogo wa Laela, Halmashauri ina Jimbo moja la Uchaguzi ambalo ni Kwela, Tarafa 4, Kata 27, Vijiji 114 na Vitongoji 463.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inategemea kilimo kwa asilimia 90%. Mazao yanayolimwa Sumbawanga ni Mahindi,Mpunga,Maharage,Karanga, Ulezi,Mtama,Mihogo na Alizeti,ambayo pia hutumika kama mazao ya biashara . Asilimia 9 ya wananchi wa Halmashauri hujishughulisha na shughuli za uvuvi katika eneo la Ziwa Rukwa na (1%) hujishughulisha na ufugaji wa nyuki na biashara ndogondogo
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa