• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

Kamati ya fedha utawala na mipango

Majukumu Ya Jumla:

Kamati hii inawashirikisha wenyeviti wa kamati zote za kudumu na inapaswa kukutana kila mwezi mara moja. Aidha, madaraka ya kamati hii ni kama kamati zingine za kudumu na hivyo hairuhusiwi kisheria kufanya kazi/majukumu ya kamati zingine za kudumu. Kwa ujumla, majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali ya Halmashauri kwa kupitia vikao vyake.

Majukumu Maalumu Ya Kamati:

 

  1. Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato.
  2. Kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na mpango wa maendeleo kwenye Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri.
  3. Kusimamia utunzia wa hesabu za fedha ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mali za Halmashauri, ukusanyaji wa mapato, kufuta madeni, na kuomba vibali maalumu kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
  4. Kufikiria na, pale inapowezekana kupendekeza kwenye Halmashauri masuala yanayohusu sheria ndogo na utendji katika ngazi za chini za Halmashauri.
  5. Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha (re-allocation) yaliyopo katika makisio yaliyoidhinishwa na kuyapeleka kwa Halmashauri.
  6. Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye kamati zingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri.
  7. Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri mikopo yote ya Halmashauri.
  8. Kutoa mapendekezo ya vitega uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa sheria ya fedha za Serikali za mitaa, sura ya 290.
  9. Kupokea na kujadili taarifa za wakaguzi wa fedha na mali ya Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya wakaguzi kwa mujibu wa sheria za Serikali za Mitaa, sura ya 290.
  10. Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Halmashauri.
  11. Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususani kuhusu taratibu za fedha, ikiwa ni pamoja na mapitia ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo kanuni mbalimbali za manunuzi ya mali na vifaa hutumika.
  12. Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali, vinavyotolewa na Halmashauri.
  13. Kufikiria na mapendekezo ya bajeti ya mipango ya maendeleo ya kila kamati ya kudumu na kuiwasilisha kwenye Halmashauri ili kupata idhini.
  14. Kushughulikia tofauti ya mapato na matumizi katika bajeti yote na kupendekeza hatua stahiki ya kuchukua kuondoa mapungufu katika mapato aua ziada matumizi.
  15. Kufikiria mapendekezo yote yanayohusu matumizi makubwa ya fedha kabla hayajawasilishwa kwenye Halmashauri ili kupata idhini.
  16. Kupokea mahesabu ya mwaka ya Halmashauri na kuhakikisha taarifa ya mahesabu ya mwaka inawasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali.
  17. Kupitia na kuidhinisha mpango wa manunuzi wa Halmashauri kwa kuzingatia mpango wa bajeti uliopitishwa na Halmashauri.
  18. Kupitia taarifa ya kila robo mwaka kuhusu manunuzi iliyowasilishwa na Afisa Masuuli.
  19. Kusimamia utekelezaji wa mikataba ya Halmashauri kwa kukagua miradi inayotekelezwa na vifaa vilivyopokelewa.
  20. Kumwelekeza Mkurugenzi kufanya manunuzi au ukaguzi wa huduma au vifaa vilivyonunuliwa ili kupata thamani halisi, itafanyika hivyo endapo itadhihirika kwamba, maelezo yaliyotolea kuhusu manunuzi ya vifaa au huduma hayaridhishi.
  21. Kuidhinisha majina ya wajumbe wa Bodi ya zabuni na wa Bodi zingine kwa mjibu wa sheria husika.
  22. Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayo wasilishwa kwenye kamati na kkutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua.
  23. Kupendekeza nja na taratibu za kuondosha vifaa chakavu. Uondoshaji wa vifaa unaweza kufanyika kwa njia ya kuuza au kuviharibu
  24. Kujadili na kupitia taarifa za fedha za kila mwezi na kila robo mwaka.
  25. Kupendekeza kwa Halmashauri hatua za kuchukua kuhusu kufuta madeni ya Halmashauri.
  26. Kushughulikiwa sera kuhusu kukopa na uwekezaji.
  27. Kujadili na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali vinavyotozwa na Halmashauri.
  28. Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine.
  29. Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya mapato ya vijiji na miji midogo kwa mujibu wa sheria, sura ya 287.
  30. Kuteua wakaguzi wa fedha / mali za Serikali za vijiji kwa mujibu wa sheria , sura ya 290.
  31. Kujadili na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua kuhusu mambo yanayohusu masuala ya ajira na kinidhamu ya wafanyakazi na watumishi.
  32. Kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yanayohusu nyumba za Halmashauri.
  33. Kupokea na kuktoa uamuzi juu ya mapendekezo ya watumishi wanaokwenda masomoni.
  34. Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya watumishi, ikiwa ni pamoja na mikopo, nyumba usafiri, matibabu, rambirambi na motisha nyinginezo.
  35. Kupitia mapendekezo ya kuthibitisha watumishi kazini baada ya kumaliza kipindi cha majaribio kulingana na miundo husika ya utumishi.
  36. Kupendekeza sheria ndogo zinazohusu kamati hizi.

Matangazo

  • Matokeo ya kidato cha nne 2022 yatangazwa. January 29, 2023
  • Matokeo ya kidato Cha pili yatangazwa. January 04, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza mwaka 2023 December 14, 2022
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa. December 01, 2022
  • Tazama

Habari Mpya

  • TAARIFA YA UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI 31 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI NA YA TATU 2022/2023 KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI MIKOPO ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA

    March 24, 2023
  • Taarifa Ya Utoaji Wa Misaada Kwa Wahitaji Siku ya Wanawake Duniani

    March 08, 2023
  • Taarifa Ya Makabidhiano Ya Safu Zamilima Ya Lyamba lyamfipa Na Msitu Wa Hifadhi Ilemba Kwa Wakala Wa Huduma Za Misitu

    February 28, 2023
  • Kikao cha Baraza Wah. Madiwani kwa aajili ya kujadili na kupitisha bajeti

    February 06, 2023
  • Tazama

Video

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dr. Haule akiwaasa Maafisa elimu kata juu ya utunzaji na matumizi sahihi ya pikipiki walizokabodhiwa
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 255755023952

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa