KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa, inapatikana Latitudi 7.9 na 9 Kusini mwa Equata na Longitudi 31 na 32.1 Mashariki mwa Greenwich,
Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga yapo eneo la Mji mdogo wa Laela, Halmashauri ina jimbo moja la uchaguzi la Kwela, kuna Taarafa 4, Kata 27, na Vijiji 114 na Vitogoji 463.
“kuboreshwa kwa hali ya maisha ya wakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kupata huduma bora na endelevu - kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia dhana ya utawala bora”.
“Kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kushirikisha wadau na wananchi katika mchakato wa maendeleo kwa kutumia rasilimali iliyopo
Eneo la Kilimo
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inakadiriwa kuwa na eneo lenye ukubwa wa hekta 620,700 ambazo kati ya hizo hekta 319,039.8 (sawa na asilimia 51.4%) ni eneo linalofaa kwa kilimo. Eneo linalolimwa linakadiriwa kuwa na wastani wa hekta 217,449.4 sawa na asilimia 68.16 ya eneo linalofaa kwa kilimo na asilimia 31.84 ya eneo linalofaa kwa kilimo halijatumika, linamilikiwa na mtu mojamoja, uwekezaji unaweza kufanyika katika eneo hili unaweza fanyika kwa kuingia ubia na wamiliki wa maeneo hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inapata mvua za kutosha, Halmashauri imegawanyika katika kanda kuu mbili, nazo ni Ukanda wa Ufipa ya Juu na Ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa.
Mahindi na Maharage hulimwa zaidi Ukanda wa Ufipa ya Juu na Mpunga na Alizeti hulimwa zaidi Ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa.
Halmashauri inatekeleza zao la Mahindi na Mpunga ni mazao ya Kipaumbele na mazao ya Korosho, Kahawa, Michikichi ni mazao ya kimkakati.
Mazao mengine yanayostawivizuri katika Halmashauri ni pamoja na ngano, mtama, ulezi, mbaazi, Karanga, mihogo, viazi vitamu na miwa.
Mazao ya Bustani yanayolimwa katika Halmashauri ni Mchicha, Kabichi, Kabichi china (Chinees cabbage), Nyanya, Biringanya, Vitunguu, Pilipili, hoho, Karoti, Nyanya, chungu, Figiri, Bamia, Ndizi, mbivu (Sweet banana), Ndizi mbichi (Plantain) na Embe Tikiti maji
SEKTA YA UMWAGILIAJI
Katika Sekta ya Kilimo cha umwagiliaji Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga inavyo vyanzo vya maji takribani 36 vyenye jumla ya hekta 31,126 katika kata 22 vilivyoainishwa kufaa kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji kwa zao la mpunga na mazao mengine ya bustani.
Miongoni mwa maeneo yanayopendekezwa kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji ni kama ifuatavyo:
Kuanzisha miundombinu katika maeneo yenye fursa au yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Ukarabati na Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.(mfano mifereji, mabwawa na visima).
Uwekezaji katika miundombinu ya uvunaji maji kama vile mabwawa, malambo, visima vifupi na virefu,n.k. pamoja na teknolojia mbalimbali za uvunaji maji.
Uzalishaji mdogo na tija.
Katika kuhakikisha kuna kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha uhakika Halmashauri ya wilaya kwa kushirikiana na serikali kuu pamoja na wadau wengine wa maendeleo ya kilimo;
Hadi sasa Halmashauri imeweza kuendeleza zaidi ya hekta 2400 kati ya heka 31,126 katika vyanzo vya maji sita(6) ambavyo ni;
Mto Mtetezi kijiji cha Ng’ongo,
Mto Mumba Kijiji cha Sakalilo,
Mto Nzovwe kijiji cha Msia,
Mto Nyombe kijiji cha solola,
Mto Vuma kijiji cha Ng’ongo na;
Mto Mbalazi kijiji cha kisa.
Kutokana na miundombinu kuendelezwa katika vyanzo hivyo uzalishaji wa zao la mpunga na mazao ya bustani umeongezeka toka tani 1 kwa hekta hadi tani 4.4 kwa hekta; hivyo kipato kimeongezeka kwa mkulima na Halmashauri kwa ujumla. Kuongezeka kwa uzalishaji inatoa fursa katika uwekezaji katika sekta ya viwanda vya kuongeza thamani kwenye zao la mpunga.
Eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri linakadiriwa kuwa na hekta 28,726 lakini bado halijaendelezwa katika vijiji 30.
Kutokana na uwepo wa eneo hilo uwekezaji katika miundombinu ya umwagiliaji kama vile mifereji, miundombinu ya uvunaji maji kama vile mabwawa, mlambo, visima vifupi na virefu,n.k. pamoja na teknolojia mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji.
NB: Maeneo yote yaliyoko kwenye vyanzo vya maji vinavyotumika kwa kilimo cha umwagiliaji yanamilikiwa kimila/ kijadi, uwekezaji katika eneo hili unaweza kufanyika kwa njia ya makubalianao/ubia na wamiliki wa maeneo.
SEKTA YA USHIRIKA
Ushirika ni sekta mtambuka kwa maana inagusa sekta nyingi kama Kilimo, Uvuvi, Fedha na Ufugaji
Fursa zilizopo kwenye sekta ya Ushirika ni kama ifuatavyo;
Idadi kubwa ya wanachama ambao wapo pamoja wapatao 3,000
Uwepo wa mashamba yanayomilikiwa na wakulima/ wanachama ambayo yanafaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali yanayoweza kuigiwa mikataba.
Uwepo wa maghala 17 ya serikali yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 11,350
Uhakika wa upatikanaji wa malighafi za kilimo kutokana na ziada ya mazao mbalimbali yanayo zalishwa katika Halmashauri hususani mahindi, Mpunga, alizeti, Karanga, Ufuta na ngano inatoa fursa ya uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao hayo
Uwepo wa soko la pembejeo ambapo mahitaji kupitia Vyama vya Ushirika kufikia shilingi 1bilioni kwa msimu.
Uwepo wa eneo lilotegwa lenye ukubwa wa ekari 7.45 Mtaa wa Ndelema katika Mji mdogo wa Laela kwa ajili ya ujenzi wa soko la mazao na maghala kwa kwaji ya kutunzia mazao
Uwepo wa eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata Mahindi, Alizeti na karanga Mji Mdogo wa Laela.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa