MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.
Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.
Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbali mbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.
Kueneza elimu ya Uraia mwema.
Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.
Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.
Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.
Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.
Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.
Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.
Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.
Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa