MIFUGO NA UVUVI.
Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ina mifugo anuai ikiwemo ng’ombe 242327, mbuzi 91266, kondoo 16723, nguruwe 14382, punda 4759 na kuku wa asili 118132 pamoja na kuku wakisasa na ndege wengine. Idadi hii inatoa fursa za uwekezaji katika Nyanja za viwanda vya uchakataji wa vyakula vya mifugo, usindikaji nyama na maziwa, uchakataji ngozi za wanyama pamoja na fursa za maeneo ya ufugaji na biashara ya ununuzi wa wanyama hai.
Ziwa Rukwa linatoa fursa ya uwekezaji kwenye mialo iliyopo na ujenzi wa mialo mipya, ufugaji samaki ndani ya ziwa (caging system) na kwenye mabwawa(fish ponds).
UFUGAJI.
Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga imegawanyika katika ukanda wa ufipa ya juu na ukanda wa bonde la ziwa Rukwa. Ukanda wa ufipa ya juu una hali la joto la wastani na maeneo ya baridi( Makuzani) yafaayo kwa kufuga ng’ombe wa maziwa kimahususi na wanyama wengine kiujumla. Maeneo ya kuchungia mifugo ni ya watu binafsi nay a jamii(communal grazing). Halmashauri inamiliki hekta 16800 eneo la bonde la ziwa Rukwa linalofaa kwa uwekezaji wa ufugaji wa kisasa na ujenzi wa viwanda vya viwanda vya kusindika vyakula vya wanyama, nyama na uchakataji ngozi.
BIASHARA YA UFUGAJI
Kuku wa kienyeji wanaweza kuwa fursa kubwa ya kibiashara ukizingatia mahitaji ya shughuli za kila siku zikiwemo sherehe. Hata hivyo pamoja na idadi kubwa iliyopo tija haiakisi vipato vya wananchi. Hii nikutokana na ufugaji wa kimazoea bila kuzingatia magonjwa na lishe. Hivyo vijana na watu wote wanakaribishwa kutumia fursa ya ufugaji bora wa kuku wa kienyeji kwa kuungana na wawekezaji wa vyakula vya mifugo ambapo nafaka(malighafi) zinapatikana kwa wingi. Fursa hii ipo pia kwenye ufugaji was nguruwe wa kienyeji ambapo wananchi wamekuwa wakiwaacha nguruwe wazurure. Hii ni fursa kwa wananchi kuwanunua nguruwe hawa wafugwao kimazoea na kuwafuga kisasa kwa kutumia fursa za ugani na vyakula zilizopo.
FURSA ZA UJENZI WA VIWANDA.
Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kusindika maziwa ya ngo’mbe wa kienyeji na wa kisasa . Kwa idadi ya ng’ombe waliopo yanapatikana maziwa wastani wa lita 300000 kwa siku. Hii inakwenda sambamba na ujenzi wa viwanda vya uchakaji na usindikaji nyama na ngozi kutokana na uwepo wa minada ya awali ya ng’ombe, mbuzi na kondoo takribani saba.
FURSA ZA UJENZI WA MIUNDO MBINU YA UFUGAJI.
Wawekezaji wana karibishwa kutumia fursa za ujenzi wa majosho binafsi kwaajili ya kudhibiti magonjwa ya wanyama pamoja na uchimbaji wa malambo ya kunyweshea mifugo.
FURSA ZA HUDUMA ZA TIBA
Wawekezaji katika uuzaji na utoaji wa huduma za tiba za mifugo wanaotambuliwa na Baraza la Veterinari Tanzania( VCT) wanakaribishwa kushirikiana na halmashauri katika kutoa huduma za veterineri(veterinary service practices).
FURSA ZA ZIWA RUKWA.
Pamoja na kutoa fursa za utalii, Ziwa Rukwa linatoa fursa ya biashara ya samaki ambayo inatoa fursa ya uwekezaji wa mialo. Ufugaji wa mamba ni fursa pia kutokana uwingi wa mamba ziwani. Wavuvi wenye boti za kisasa wanakaribishwa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa