Naibu Waziri Wizara ya TAMISEMI Mh. David Silinde ametembelea miradi ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga leo tarehe 26/11/2021 na kukagua baadhi ya miradi inayojengwa katika Halmashauri hiyo, miradi aliyotembelea ni ujenzi wa madarasa 6 shule ya sekondari Uchile kata ya Kasanzama wenye thamani ya shilingi 120,000,000 na Shule ya Sekondari Mpui iliyoko kata ya Mpui madarasa 8 wenye thamani ya shilingi 160,000,000
Aidha katika ziara hiyo, Mh. Naibu Waziri alilisisitiza kuwa, miradi inatakiwa ikamike kwa haraka kabla ya shule kufunguliwa kwa mwaka 2022, pia alilisistiza thamani ya miradi iakisi uhalisia wa pesa iliyotolewa(Value for money) kwa kila mradi.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Sebastian Waryuba aliongezea kuwa ametoa maelekezo kwa miradi yote inayotekelezwa ili ikamilike kwa wakati na kwa tija.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa