Waziri wa Nishati Mh. DKT. Medard Kalemani amefanya ziara ya kugagua mradi wa upelekaji wa umeme katika kata ya Milepa iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kituo cha afya milepa. Ziara hiyo imefanywa siku ya Jumanne tarehe 27/08/2019 katika viwanja vya Milepa.
Baada ya kukagua mradi huo Mh. Waziri alipata fursa ya kuongea na wananchi wa kata ya Milepa Waliokuwa wamehudhuria kwenye mkutano huo. Mh. Waziri alielezwa na Diwani wa kata hiyo Mh. Apornali Macheta kwamba wananchi wa kata ya Milepa wanashauku kubwa ya kupata umeme kwenye kata yao kwa kuwa kata yao ni miongoni mwa kata ambazo zinakua kwa kasi na wananchi wake wanajituma katika shughuli za maendeleo ambazo zinahitaji uwepo wa nishati ya umeme.
Mh. Diwani wa kata ya Milepa alimweleza Mh. Waziri kuwa pia kuna kituo cha Afya Milepa ambacho ni kituo kikubwa ambacho nacho kinahitaji uwepo wa nishati ya umeme lakini mpaka sasa bado shirika la Tanesco halijaweka umeme.
Baada ya kumsikiliza Mh. Diwani wa kata ya Milepa, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Mh. Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Mh. Waziri wa Nishati Mh. DKT. Medard Kalemani alitoa maagizo yafuatayo kwa uongozi wa Tanesco:-
Mwisho aliwataka wananchi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha Tanzania ya Viwana inawezekana kwa kiwango kikubwa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa