Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma husherehekewa kila mwaka na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa lengo la kuonesha mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya Nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga maadhimisho hayo yamefanyika siku ya Jumatano tarehe 17/07/2019 katika ukumbi wa Halmashauri na mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Utumishi kutoka ofisi ya RAS ambaeye anaitwa Bi. Winifrida Kijazi.
Mgeni rasmi alianza kwa kuwakaribisha watumishi waliofanikiwa kuhudhulia maadhimisho hayo na kisha kuwataka wawe huru na wawazi katika kutoa kero zao. Aliwaeleza kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji, Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi,”
Aliwakumbusha watumishi kanuni za maadili ya utendaji wa shughuli za kiserikali. Alisisitiza pia suala la utunzaji wa siri. Aliwataka watumishi wanaohusika na masijala ya wazi kuwa makini sana katika utunzaji wa nyaraka zao.
Baadhi ya watumishi waliwasilisha kero mbalimbali ikiwemo kutokupanda madaraja, nyongeza ya mshahara, madai ya likizo, wastaafu kucheleweshewa mafao yao kero ambayo ilionekana ni yenye kuumiza zaidi kwa kuwa mtumishi amestaafu hana fedha ya kuendeshea maisha lakini bado anakaa muda mrefu bila kupata mafao yake. Na kero hii iliongelewa kwamba imekuwa kubwa zaidi hasa baada ya kuuganishwa kwa mifuko ya jamii. Lakini pia waliongelea changamoto za bima ya afya ambazo watumishi wanapohitaji huduma kama kadi kutokutambulika, baadhi ya dawa kutokupatikana n.k.
Mgeni rasmi alizipokea kero hizo na alitoa ufafanuzi kwa baadhi ya kero na nyingine akaahidi kuzifikisha mahala husika ili ziweze kufanyiwa kazi. Lakini pia aliwataka watumishi kutimiza wajibu wao kwanza kabla ya kudai haki zao.
Mgeni rasmi alihitimisha maadhimisho hayo kwa kuelezea kuhusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu. Aliwataka watumishi watakaohusika na zoezi la usimamizi wa uchaguzi huo kuwa waaaminifu na waadilifu na wenye kutambua wajibu wao na majukumu yao.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa