Jumla ya wanafunzi 759,706 sawa na asilimia 91.1 ya wanafunziwaliofaulu wakiwemo wavulana 368,174 na wasichana 391,532 wamechaguliwakujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021.
Kaulihiyo imebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akitoa taarfa ya uchaguzi wawanafunzi wa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2021 leo jijiniDodoma.
AkizungumzaMhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi 4,169 wamechaguliwa kujiunga na shuleza bweni ambapo wanafunzi 970 watajiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulumzuri Zaidi.
PiaMhe. Jafo amesema kuwa wanafunzi 1,238 watajiunga na shule za ufundi, wanafunzi1,961 watajiunga na shule za bweni za kawaida.
Wanafunzi755,537 wakiwemo wavulana 362,247 na wasichana 385,665 wamechaguliwa kujiungana shule za Sekondari za kutwa katika maeneo mbali mbali nchini.
“Miongonimwa waliochaguliwa, wanafunzi wenye mahitaji maalum ni 2,491 wakiwemo wavulana1,312 na wasichana 1,179 sawa na asilimia 75.0 ya wanafunzi wenye ulemavuwaliofanya mtihani huo.
Mhe.Jafo ameeleza kuwa jumla ya mikoa tisa ya Kagera, Katavi, Lindi, Mtwara,Mwanza, Njombe, Ruvuma, Songwe na Tabora imeweza kupangia shule wanafunzi wotewaliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.
Hatahivyo jumla ya wanafunzi 74,166 sawa na asilimia 8.9wakiwemo wavulana 34,861 nawasichana 39,305 hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhabawa vyumba vya madarasa.
“Hivyowanafunzi wenye sifa ambao hawakupangiwa shule katika awamu hii ya kwanzawatapangiwa shule katika awamu ya pili kabla ya tarehe 28 Februari, 2021”,ameeleza Mhe. Jafo
Kwakuongezea Mhe. Jafo amesema kuwa wanafunzi hao wataendelea kupangiwa shulekadri Mikoa na Halmashauri zitakavyoendelea kukamilisha vyumba vya madarasa namadawati hadi kufikia tarehe 28 Februari, 2021.
Aidhaamewaagiza walimu na watendaji wa sekta ya Elimu katika ngazi zote kuongezabidii katika usimamizi na ufuatiliaji wa utoaji wa elimu ili kufikia malengo yaelimu yaliyopangwa na serikali.
“Ninatoawito kwa viongozi wa Mikoa na Halmashauri kushirikiana na wadau wa elimukukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wotewaliochaguliwa kuanza masomo yao mwezi Januari, 2021 bila vikwazo vya ainayoyote”, ametoa wito Mhe. Jafo.
Vilevile amesema kuwa wakuu wa mikoa na halmashuri kuhakikisha wanafunzi wotewanaripoti shuleni kwa wakati.
Mhe.Jafo amesema kuwa mzazi au mlezi ambaye atakuwa na hoja yoyote juu ya uchaguziwa wanafunzi afike Ofisi za Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri husika iliaweze kuhudumiwa ipasavyo.
Aidhaanaweza kupiga simu katika kituo cha huduma kwa wateja katika Ofisi ya RaisTAMISEMI kwa namba ya simu 026-2160210 AU atume ujumbe mfupi wa (SMS) auWhatsApp kwa namba ya 0735160210
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa