Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imetoa miezi mitatu kwa Wakurugezni wa halmashauri zote nchini kuhakikikisha wanatoa mikoipo inayokidhi vigezo vya kibaiashara kwa makundi ya wanawake waliopo kwenye maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo Mh.Ummy Mwalimu katika kilele cha maazimisho ya Siku ya wanawake Duniani kilichofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri Mwalimu alisema wapo baadhi ya Wakurugenzi wanaopuuzia kutoa mikopo hiyo ihali wakifahamu kuwa serikali ilipita na kutoa ahadi kwa wanawake kuwa itawezesha kiuchumi kwa kuwapa mikopo hiyo ambayo inatokana na mapato ya ndani ya halmashauri.
"Mimi kama Waziri mwenye dhamana nasubiri hadi Juni 30, mwaka huu na iwapo kutakuwa na Mkurugenzi ambaye hatatoa mikopo kwa wanawake kwenye eneo lake basi nitachukua majina yao na kuyapeleka kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli ili aweze kuwachukulia hatua za kupuuza agizo hilo".Alisema Waziri huyo
Aidha Waziri Mwalimu alikemea tabia ya baadhi ya Wakurugenzi ambao wamekuwa wakitoa mikopo kiduchu kwa wanawake, kiasi kwamba inawawia vigumu kufanya biashara walizokusudia.
Alisema..."Utakuta Mkurugenzi anatoa mkopo wa kiasi cha shilingi laki tatu kwa kundi la wanawake sita , eti ili wagawane kila mtu shilingi elfu hamsini, hivi elfu hamsini unaweza kufanya biashara gani jamani? Na ndio maana hiyo mikopo wakitoa inashindwa kurejeshwa kwa sababu hao wanawake wanaamua kuzitumia kwa matumizi mengineyo fedha hizo."
Alisema mikopo inayotolewa lazima ilenge kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi na kuendana na hali halisi ya uchumi wa viwanda ambapo mkakati uliopo unalenga sana katika kumwezesha mwanamke aliyepo vijijini
(Picha na habari na Simon L. Kisika)
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa