Mwenge wa uhuru umezindua, kuweka jiwe la msingi na kukagua miradi mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1,449,073,079 uliokimbizwa 7/4/2019 katika halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga
Aidha miradi hiyo iliyowekea jiwe la msingi, kukaguliwa na kuzinduliwa ni Jengo la huduma ya wakala NMB lenye thamani ya TSh 42,300,000, Nyumba ya walimu(six in one) yenye thamani ya shs 174,977,775, Uanzishwaji wa shule ya sekondari kapenta yenye thamani ya shs 208,627,000, Klabu ya mapambano dhidi ya rushwa na madawa ya kulevya wenye thamani y ash 1,986,000, Ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao kijiji cha Sakalilo lenye thamani ya sh 101,200,000, Ujenzi wa shule ya msingi Maenje yenye thamani ya sh 73,000,000, Uboreshaji wa miundombinu kituo cha afya Milepa chenye thamani ya sh 438,739,000, mradi wa maji ya mserereko kijiji cha Msia wenye thamani ya sh 370,641,304, shamba darasa la Alizeti lenye ukubwa wa ekari 20 thamani yake sh 6,584,00
Pia kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg Mzee Mkongea Ally katika kata ya Muze wilayani humo alikabidhi mikopo wanawake, vijana na walemavu sh 20,000,000, zawadi kwa shule za msingi na sekondari zilizofanya vzuri sh 3,000,000, vyandarua kwa wazee vyenye thamani y ash 1,000,000, ugawaji wa vitambulisho kwa wazeevyenye thamani ya sh 320,000, kukabidhi mizinga 15 ya nyuki na seti 5 za mavazi ya kinga yenye thamani ya sh 2,000,000 na kutoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wenye thamani y ash 4,698,000
Aidha, wakati akitoa ujumbe wa Mwenge katika kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta wilayani humo, kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg Mzee Mkongea Ally aliwaasa wanachi walinde vyanzo vya maji kwa kutokukata miti na kulima kwenye vyanzo vya maji.
Pia aliongeza, kwa kuwa mwaka 2019 ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wananachi wanatakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali na kuchagua watu waadilifu na siyo kuchagua watu waliotoa rushwa kwa kuwa wagombea wanaotoa rushwa hawatawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa