Mkuu wa wilaya Mh. Sebastian Waryuba Mgeni rasmi akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Sumbawanga pamoja na Mganga mkuu wa wilaya kwenye matukio mawili moja Uzinduzi wa chanjo ya polio, pili uzinduzi wa Zahanati mbili Zahanati ya Lyapona iliyopo kata ya Kanda na Zahanati ya Kizumbi iliyopo kata ya Lusaka.
Mgeni rasmi alitoa elimu juu ya faida za polio na madhara yanayoweza kutokea kwa watoto ambao hawatapata huduma hiyo. Hivyo aliwashauli wananchi kutoa ushirikiano kwa wauguzi wa afya wanaotoa huduma hiyo wilaya nzima ili kila mtoto alie na umri chini ya miaka mitano afikiwe na huduma hiyo.
Pia mgeni rasmi aliongelea swala la upandaji wa miti ili kuendelea kuyaweka mazingira katika hali nzuri. Maana miti ni uhai. Tunza mazingira nayo yakutunze.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa