Mkuu wa wilaya ya Sumbawawanga Dr Khalfani Haule ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vya Sandululu, Mpwapwa na Msandamuungano kutumia fursa ya kampeni ya uhamasishaji kwa wananchi kuchukua hatua ya kupima maeneo yao, ili kupata hati za kimila. Wito huu umetolewa katika viwanja vya mpira wa miguu vilivyopo kijiji cha Jangwani kata ya Sandulul
Mh. Mkuu wa Wilaya amesema baada ya kukamilika kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi wananchi wanahamasishwa kuhakikisha wanapima maeneo yao ili kuweza kupewa hati za haki za kimila.
Pia Mh. Mkuu wa Wilaya aliwaeleza wananchi faida za kumiliki maeneo yao ikiwa ni pamoja na uhakika wa umiliki wa eneo, kuongeza thamani ya ardhi, kuondoa au kupunguza migogoro ya ardhi na ardhi kutumika kama dhamana.
Kampeni hiyo inatekelezwa na shirika la MIICO ambalo linatekeleza mradi wa ushawishi wa upatikanaji wa ardhi bora kwa wazalishai wadogo katika Wilaya ya Sumbawanga, vijiji vya Sandululu, Mpwapwa na Msandamuungano.
Mradi umewajengea uwezo wananchi katika kutambua sheria mbalimbali za ardhi na matumizi bora ya ardhi na matumizi bora ya ardhi. Kupitia mradi huu wananchi mbalimbali wameweza kutambua umuhimu wa kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi, ambapo vijiji vya Sandulula, Jangwani na Mumba vimeweza kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi. Baada ya kukamilika kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi wananchi wanahamasishwa maeneo yao kwa kupewa hati za haki za kimila.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa