• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

UTOAJI WA MIKOPO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

Tarehe ya kuwekwa: July 4th, 2021

UTOAJI WA MIKOPO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

Mifuko ya Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Walemavu ilianzishwa kwa ajili ya kutoa Mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Mifuko hii  inaendeshwa chini ya Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu za mwaka 2019; kanuni hizi zimetungwa kwa lengo la kutekeleza sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa sura Na. 20 chini ya Kifungu cha 37A (4).

Chini ya Kanuni hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) inakuwa na wajibu wa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kiasi hicho kilichotengwa hutolewa kwa Vikundi Vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa vigezo vilivyoainishwa katika kanuni hizo.

Utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2020/2021

Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashari ilitenga jumla ya shilingi 241,000,000 kama sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri fedha hiyo ilipangwa kutolewa kwenye vikundi 60 vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu .

Kwa kipindi cha Julai 2020 hadi  30 Juni,  2021 Jumla ya vikundi 24 vyenye wanachama 217 vinapewa mikopo yenye thamani ya shilingi 114,000,000; kati ya vikundi  hivyo  Vikundi 12 ni vya wanawake ambao idadi  yao ni 148, vikundi 8  ni vya vijana ambao wako 69 na vikundi 4 ni vya walemavu.

Kiasi hiki cha mikopo  ya shilingi milioni 117,000,000 kinafanya jumla ya mikopo iliyotolewa kwa mwaka huu wa fedha kuwa shilingi milioni 152,000,000 ikiwa na pamoja na mikopo ya shilingi milioni 35,000,000 iliyotolewa kwa vikundi 8 katika robo ya tatu ya mwaka huu (2020/2021)

Ufuatiliaji wa marejesho kwa mwaka 2020/2021

 

Kwa mwaka wafedha 2019/2020  Halmashauri ilikopesha jumla ya shilingi 175,000,000 kwenye vikundi 40 vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu,  hadi kufikia  30 Juni 2021 katika fedha hizo  Shilingi  98,500,000 zimerejeshwa kutoka vikundi 40 vilivyokopeshwa. Aidha marejesho yanaendelea  kukusanywa kwani vikundi vingi bado viko ndani ya muda wa mkataba. 

 

Changamoto

Bado kuna Baadhi ya Vikundi havirejeshi  fedha za mikopo kwa wakati kulingana na mikataba; hii inasababisha kuchelewa kutoa mikopo kwa wahitaji wengine. Ili kukabiliana na changamoto hii, tutaendelea kufanya yafuatayo:-

  • Kutoa elimu ya ujasiliamali kwenye vikundi vyote vya wajasiliamali vinavyopewa mikopo.
  • Tunaendelea kufanya ufuatiliaji wa marejesho ili vikundi kuweza kurejesha mikopo kwa wakati.
  • Elimu ya uundaji na uendeshaji wa vikundi inaendelea kutolewa
  • Tunaendelea kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Ofisi ya OCD kufuatilia madeni sugu.

 

Mkakati kwa 2021/2022

Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashari imejiwekea mikakati  ya kuhakikisha kuwa inaongeza ukusanyaji wake wa mapato ya ndani na utoaji wa mikopo  kwa wingi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa kufanya yafuatayo :-

 

  • Kufanya mikutano na kundi la Watu Wenye Ulemavu ili wahamasike kujiunga katika vikundi na kuanzisha shughuli za ujasiliamali na kuzifikia huduma za Mfuko wa Mikopo wa Walemavu
  • Kufanya mafunzo elekezi kwa vijana wenye ujuzi wa ufundi Mchundo  ukiwemo wa uashi, uselemala, kufyatua matofali kwa kutumia saruji, umeme, n.k. ili waweze kuunda vikundi vya uzalishaji mali. Vikundi hivyo vitaunganishwa na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu
  • Kubaini wabunifu wa shughuli mbali mbali za ufundi na biashara mbali mbali katika makundi haya ya Vijana, Walemavu na Wanawake ili kuwaunganisha na huduma za kifedha
  • Kufanya ufuatiliaji wa urejeshaji wa Mikopo na kuendelea kujenga uwezo kwa vikundi

Matangazo

  • Baraza la Mitihani Tanzania latangaza matokeo ya darasa la saba 2024 October 29, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Orodha ya asasi zilizopata kibali cha uangalizi wa uboreshaji wa daftari mwaka 2024/2025 June 26, 2024
  • Tazama

Habari Mpya

  • Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

    September 05, 2024
  • Makabidhiano ya ofisi

    August 21, 2024
  • CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

    July 25, 2024
  • Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa

    May 25, 2024
  • Tazama

Video

Kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 0754634811

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa