Wakulima na wafugaji wametakiwa kutumia fursa ya maonyesho ya nanenane kuweza kuongeza uzalishaji ili kukuza pato kwa familia na Serikali kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.
Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh.Mwita Waitara ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Manonesho ya Nane Nane 2019 kanda ya nyanda za juu kusini kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 03/08/2019.
Amesema elimu inayotolewa kwenye maonyesho hayo na wataalamu wa kilimo na mifungo iwe ni chachu kwa wakulima na wafugaji ili kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Vile vile amewataka wataalamu wa kilimo hapa nchini kuhakikisha elimu na mafunzo yanayotolewa kwenye Maonesho ya Nane Nane yanawafikia wakulima na wafugaji waliopo vijijini ambao hawajapata fursa ya kufika kwenye maonyesho hayo.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh. Mwita Waitara amesema baada ya kutembelea mabanda mengi kwenye maonyesho hayo amebaini kuna ubunifu na utaalamu mkubwa uliopo kwenye sekta ya kilimo na mifugo lakini bado hauwanufaishi wakulima na wafugaji walio wengi.
Mh.Waitara amesema Halmashauri na wajasiriamali wengi wameweka vitu mbalimbali kwenye maenesho hayo, lakini anapata mashaka iwapo maarifa hayo yanatumika ipaswavyo katika kuhakikisha wakulima wanalima kwa kuzingatia taratibu huko walipo hususan maeneo ya vijijini.
Aliwataka wakuu wa Mikoa kusimamia uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo, tume ya ushirika kuanzisha na kusimamia vyama vya kukopa (SACCOS). Pia akawaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya akina mama, vijana na walemavu ili waweze kuwekeza kwenye kilimo.
Mwisho aliwaeleza wananchi kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo basi akawataka watumie haki yao ya kimsingi ya kupiga kura kwa mgombea watakae ona anawafaa.
Maadhimisho hayo ya sherehe za nanenaen kanda ya nyanda za juu kusini yanahusisha mikao ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa