Mifuko ya Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ilianzishwa kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemvu. Mifuko hii inaendeshwa chini ya Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2019 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2020; Kanuni hizi zimetungwa kwa ajili ya kutekeleza Sheria ya Fedha ya Seikali za Mitaa syra Na. 20 Kifungu cha 37A (4).
Kanuni hizo zimetoa wajibu kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) kutenga asilimia 10 ya mapato yake yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani (Own Source) kwa ajili ya kuwezesha mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambao nao hukopeshwa kwa mujibu wa masharti yalitolewa na kanuni hizo.
UTENGAJI NA UTOAJI WA MIKOPOKWA VIKUNDI VILIVYOSAJILIWA VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU MWAKA 2022/2023
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilipanga kutoa shilingi 268,750,000/= ambayo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Hadikufikia leo, Halmashauri imetoa shilingi 169,200,000/= ikiwa ni sehemu ya asilimia kumi ya kiasi kilichokisiwa kutolewa sawa na asilimia 63 ya lengo. Mchango huu wa asilimia kumi umewezesha kutoa mikopo ya jumla ya shilingi 373,750,000 kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023 inayotokana na mchango wa asilimia kumi ya mapato ya ndani ya mwaka huu wa fedha (shilingi 169,200,000/= ) na fedha inayotokana na marejesho (shilingi 204,550,000/=).
Ili kuweza kukamilisha mchakato wa utoaji wa mikopo; shughuli zilifanyika ni pamoja na
Wanavikundi kuomba mikopo kwenye Mfumo wa kielektoniki wa Utoaji na Usimamizi wa Mikopo ya Halmashauri ya Asilimia kumi maarufu kama TPLMIS,
Uidhinishaji wa mikopo katika vikao vya Kamati za Mikopo ya Halmashauri, CMT na Fedha, Uongozi na Mipango.
Utoaji wa Mafunzo kwa vikundi;
Ulipaji wa fedha katika akaunti za vikundi;
Usainishaji wa mikataba ya vikundi na
Makadhiano ya mikopo kupitia hafla hii ya kukabidhi mikopo.
Mafunzo kwa vikundi
Kwa robo hii ya Tatu ya mwaka 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imefanikiwa kutoa mafunzo ya ujasiliamali na mikopo kwa vikundi 32 vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu vilivyokuwa na washiriki 114. Mafunzo yalikuwa ya siku tatu tarehe 12 hadi 14 Machi, 2023. Wawezeshaji wa mafunzo walikuwa wataalamu kutoka Ofisi ya Maendeleo ya jamii, Biashara, Kituo cha kilimo Laela na SIDO.
Ulipaji wa fedha katika akaunti za vikundi
Shughuli ya kuingiza fedha (kulipa) katika akaunti za vikundi imekamilika. Hadi sasa vikundi 31 vimeingiziwa jumla ya shilingi 268,750,000/= katikaakaunti zao. Mikopo hii inawawezesha wanavikundi kutekeleza miradi waliyoombea mikopo na kuidhinishwa na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango.
Miradi iliyokopewa na kuidhinishwa ni pamoja na
Vikundi vitano vimeweza kukopeshwa mashine sita (6) yaani mashine ya kusaga mahindi, mashine mbili za kukamulia alizeti, mashine ya kutengeneza sabuni, mashine ya kutotoreshea vifaranga vya kuku na mashine ya kuchakata chakula cha mifugo
Pikipiki 14 aina ya kinglion
Vikundi vilivyobaki vimeomba shughuli ya kuongeza mitaji ya vikundi kwa ajili ya kukopeshana na biashara ya mazao.
Manunuzi ya mashine hizo yanafanywa na wanavikundi wenyewe na mpaka sasa vikundi vyote vimemaliza kufanya manunuzi na mara baada ya kukabidhiwa mikopo wataanza utekelezaji.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa