Safu zamilima ya Lyamba lyamfipa zipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na zina ukubwawa 244,101 Hekta kutoka Mfinga hadi kijiji cha Mkowe kata ya Miangalua. Safuhizi zinapakana na vijiji 42 na katika safu hizi ipo hifadhi ya msitu wa Ilemba pamoja na vyanzo vya maji (mito) vinavyopeleka maji Ziwa Rukwa. Vyanzo hivi vya maji vinategemewa na vijiji kwa ajili ya huduma ya maji ya matumizi ya nyumbani na kilimo cha umwailiaji, lakini pia vyanzo hivi ndivyo vinategemewa kujaza maji katika ziwa Rukwa.
Changamoto zilizopo katika safu za milima ya lyamba lyamfipa
Safu hizi zina kabiliwa na uvamizi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji,na ukatajimiti. Pia ucho maji moto na uharibifu wa vyanzo vya majina bioanuai zilizopo katika misitu.
Kutokuwepo kwa mipaka ya hifadhi ya safu za lyambalyamfipa
Eneo la safu ya milima ya Lyamba lyamfipa kupimwa kama sehemu ya vijiji vinavyo zunguka safuhizi.
Halmashauri kutokuwa na Rasilimali pamoja na wataalam wa kutosha kwa ajili ya usimamizi na uhifadhi wa safuhizi.
Kutokana na changamoto hizo Halmashauri iliagizwa na Kamati ya Ushauri Mkoa na Wilaya pamoja na Baraza la Madiwani kufanya taratibu za kukabidhi safu za milima ya Lyambalyamfipa na Msitu wa Hifadhi Ilemba kwa wakala wa huduma za Misitu ili uweze kusimamiwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Menejimenti ya Halmashauri imefanikiwa kufanya mikutano ya Hamasa katika Vijiji 30 vinavyozunguka safu hizi kwa ajili ya kuwajulisha adhma hii ya kukabidhi safu hizi kwa ajili ya kuhifadhiwa na kuzuia uharibifu. Wananchi walio wengi wameridhia na kutaka kushirikishwa wakati wa kuweka mipaka, kazi ambayo itafanywa kwa pamoja na wakala wa Huduma za Misitu.
Safu za Milima ya Lyambalyamfipa zinapakana na Halmashauri tatu ambazo ni Sumbawanga Vijijini, Sumbawanga Mjini pamoja na Wilaya ya Nkasi.
Hifadhi ya safu za Milima ya Lyambalyamfipa upande wa Sumbawanga Vijijini imezungukwa na Kata zifuatazo; Mfinga, Mwadui, Kalumbaleza, Muze, Zimba, Mtowisa, Milepa, Ilemba, Nakanga, Kapenta, Miangaluwa pamoja na Kaoze. Katika safu za Milima ya Lyambalyamfipa kuna Msitu wa hifadhi wa Ilemba (Ilemba local Authority Forest Reserve) Ulioanzishwa 1959 na kutangazwa kwenye gazeti la serikali GN 363/13/10/1961. Safu za milima ya Lyambalyamfipa zina ukubwa wa hekta 244,101 ambapo ndani yake kuna msitu wa Hifadhi wa Ilemba wenye hekta 4923.
Ushirikishwaji Wa Wananchi Kwenye Vijiji Vinavyopakana Na Safu Za Lyambalyamfipa
Halmashauri kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za misitu wa lifanya mikutano katika vijiji vinavyo pakana na safu za Lyamba lyamfipa kwa lengo la kutoa hamasa na kuwajulisha wananchia dhama ya Halmashauri kukabidhi safu za Lyamba lyamfipa kwa Wakalawa Huduma za Misitu ili ziweze kuhifadiwa vyema.
Mipaka ya awali ili chukuliwa kwa GPS kwa kushiriana na viongozi wa Vijiji, viongozi wa Kata ,Wazee Maarufu na baadhi ya wananchi wanaojua maeneo ya vijiji vyao.
Wadau Wanaofanya Kazi Za Uhifadhi Katika Safu Za Milima Ya Lyambalyamfipa Na Msitu Wa Hifadhi Wa Ilemba
Wapo wadau mbalimbali wanaofanya kazi za uhifadhi katika safu za milima ya Lyambalyamfipa na Hifadhi ya Msitu wa Ilemba kwa kushirikiana na Halmashauri kama ifuatavyo;
Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira ambao wanatekeleza Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili katika Vijiji 11 vya Kata za Muze, Kalumbaleza na Mwadui. Mradi huu pamoja na uhifadhi wa Maliasili umefanya mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji vyote vya Kata hizi.
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kushirikiana na Halmashauri wanatekeleza Mradiwa Urejeshwaji wa bioanuai na hifadhi ya mazingira katika Kata za Ilemba, Nankanga na kapenta.
Halmashauri inashauri wadau hawa waendelee na kazi za uhifadhi katika maeneo haya ili kazi kubwa iliyofanyika isiathirike na mabadiliko haya.
Mapendekezo Ya Halmashauri Katika Kuhifadhi Safu Za Milima Ya Lyambalyamfipa
Kushirikisha vijiji wakati wakupitia mipaka ya hifadhi na usimamizi wa safu za milima ya Lyambalyamfipa pamoja na msitu wa hifadhi wa Ilemba.
Eneo la kata za Muze, Kalumbaleza na Mwadui ambalo lipo chini ya Mradiwa Usimamizi Endelevuwa Maliasili liendelee kusimamiwa kwa pamoja na vijiji kutokana na kazi kubwa ya uhifadhi inayoendelea kufanyika.
Baada ya mipaka kuwekwa, tunashauri wakala wa Huduma za Misitu afanye mchakato wa kuanzisha biashara ya Hewa Ukaa.
Kama mchakato wa kuanzisha biashara ya hewa ukaa ukifanikiwa, Halmashauri na vijiji vinavyopakana na safu za Lyambalyamfipa ifaidike na Mapato yatakayotokana na biashara ya hewa ukaa kwa asilimia 50.
Usimamizi wa safu za milima ya Lyambalyamfipa ufanyike kwa njia shirikishi (usimamizi shirikishi).
Kitongoji cha matoto kilichopo Kata ya Zimba ambacho kimeanzishwa ndani ya msitu na kando ya chanzo cha maji kiondolewe.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa