Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sumbawanga Ndg. Kalolo Ntila ameagiza watalaamu wa Halmashauri hiyo kufanya utafiti wa kilimo cha mazao ya kahawa na korosho
Ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani kilichoketi 28/05/2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga.
Ameongeza kwa kuwa mazao ya chakula yanayolimwa katika Halmashauri ambayo pia huuzwa na wananchi kwa ajili ya kujipatia pesa yameshuka bei, ni wakati mwafaka kwa wataalam wa Idara ya Kilimo kufanya utafiti wa mazao ya Kahawa na Korosho kwa kuwa hali ya hewa ya Halmashauri hiyo imegawanyika, ukanda wa juu ambao ni wa baridi na bondeni ambao ni wa joto. Aliongeza kuwa, uanzishwaji wa mazao hayo ya biashara utasaidia kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na Halmashauri kwa ujumla.
Pia alisema, hadi kufikia 30 March 2018, Halmashauri imeweza kukusanya sh 1,563,211,402 dhidi ya 2,399,406,000 sawa na 65% ya lengo la mwaka 2017/2018. Kuongezeka kwa vyanzo vya mapato na ukusanyaji utasaidia Halmashauri iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari katika vijiji na kata mpya.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa