Mkuu wa wilaya ya Sumbawawanga Dr Khalfani Haule amekabidhi pikipiki ishirini na saba zenye thamani ya shilingi milioni tisini na nne kwa maafisa elimu kata, tukio hilo limefanyika August 15, 2018 katika ofisi za Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga
Amesema serikali imekuwa na mpango wa kuwanunulia waratibu elimu kata pikipiki kupitia mpango wa LANES(Literacy and Numerus Education Support) lengo kubwa la mpango huu ni kukuza stadi kuu tatu za kusoma, kuhesabu na kuandika (K.K.K) katika shule za msingi.
Pia amewataka maafisa elimu kata wakasimamie ufaulu kwa kuwa tayari wana vyombo vya usafiri.”Fuatilieni wanafunzi watoro na muwarudishe shuleni”
Katika suala la utunzaji wa pikipiki amewataka wazitunzwe katika kiwango kinachotakiwa ili zibaki na hali yake ya uimara na zitumike katika malengo yaliyokusudiwa
Dr. Haule pia amewataka wakakamilishe ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwa kila shule ili kupunguza msongamano wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya kwa vijiji ambavyo havina shule.
Pia amwataka waache tabia ya kufukuza wanafunzi kwa sababu ambazo hazina msingi, zaidi kuwahimiza washirikiane na jamii iliyopo ili kuongeza tija ya ufaulu kwa wanafunzi
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa