Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Queen C. Sendiga akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Sumbawanga na Mkoa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wametoa msaada wa kibinadam kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea kijiji cha Kasekela na Msila Kata ya Mfinga. Misaada iliyotolewa ni:- Misaada ilivyokabidhiwa ni pamoja na Maharage kilo 1120, unga wa sembe kilo 1440, Mafuta ya kupikia lita 154, mikeka 21, vyandarua 20, mablanketi 21, Sufuria za kupikia 21, na miche ya miti 250 kwa ajili ya kupanda ili kurudisha uoto wa asili unaozidi kupotea.
Baada ya kutoa msaada huo, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amewaagiza wananchi wa Kijiji cha Msila, Kasekela na wananchi wote wa Mkoa wa Rukwa kuondoka na kuacha kulima kandokando ya mito kwa hiyari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa shuruti. Amewaambia wananchi hao kuwa mafuriko na mabadiliko ya tabia nchi yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika kandokando ya mito, milimani na katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.
Kiongozi huyo wa Mkoa ameitaka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kutafuta dawa kwa ajili ya kutibu maji baada ya kupokea maombi ya wakaazi wa vijiji hivyo vilivyoathiriwa na mafuriko. Amemwelekeza Meneja wa Mamlaka hiyo Wilayani Sumbawanga kuhakikisha maji ya visima vilivyopo yanatibiwa ili wananchi wapate maji safi na salama kwa haraka wakati mradi mkubwa wa maji unaoendelea kutekelezwa kwa awamu ukiendelea.
Baada ya zoezi hilo kukamilika alitembelea na kukagua zahanati ya Uzia kata ya Muze na Hospitali ya Wilaya iliyojenga kata ya Mtowisa ili kukagua mwenendo wa ujenzi unaoendelea kwenye majengo hayo.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa