Mwenge wa Uhuru ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Tangu kuanzishwa kwa mbio hizi, Mwenge wa Uhuru umekuwa kichocheo kikubwa katika kuimarisha Uhuru wa Nchi, Umoja wa Kitaifa, Kudumisha Amani, kulinda Muungano na Kuhamasisha Maendeleo ndani na nje ya Nchi yetu.
Mbio za Mwenge wa uhuru 2022 katika Wilaya ya Sumbawanga, umekimbizwa kilometa 178.5 katika maeneo mbalimbali na utafanya kazi za kuweka jiwe la msingi, kukagua utoaji wa mikopo na kutoa motisha. Thamani ya miradi yote iliyokaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi, utoaji wa mikopo na utoaji wa motisha ina jumla ya Tsh 1,136,689,000
Mwenge wa Uhuru umepokelewa siku ya Jumatatu tarehe 19/09/2022 katika Kijiji cha Kipeta ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma, na utapita katika vijiji vya Kilyamatundu, kipeta, Chombe na Laela.
Mwenge ukiwa Kipeta Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alikagua na kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha Afya kipeta. Mradi huu ulipata fedha za tozo kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi 500,000,000 ambazo zilipokelewa kwa awamu mbili tofauti, kwa ajili ya kujenga majengo matano (5) ambayo ni Jengo la Wagonjwa wa nje OPD, kichomea taka ngumu (Incinerator), jengo la Maabara, wodi ya wazazi, jengo la upasuaji.
Mwenge ukiwa Kipeta Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alikagua Klabu ya wapinga Rushwa na dawa za kulevya katika shule ya Sekondari Kipeta kilichoanzishwa mnamo tarehe 10/01/2020 ikiwa na wanachama wapatao 20, kwa madarasa yote yaani kuanzia kidato cha I-IV, hadi sasa Klabu ina wanachama 35 (wavulana 20 na wasichana 15). Klabu hii imeundwa na inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria ya kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 iliyoipatia TAKUKURU jukumu la kuongoza na kushirikiana na makundi yote ya jamii katika mapambano hayo.
Mwenge ukiwa Laela Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alikagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Shule ya sekondari Katuula. Tarehe 28/12/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kupitia Shule mama ya Sekondari ya Uchile ilipokea fedha Tsh.470,000,000 za utekelezaji wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Katuula. Fedha hizi ni kwa ajli ya ujenzi wa madarasa nane (8), Jengo la utawala, Maabara tatu (3), Chumba cha ICT, Maktaba pamoja na matundu ishirini (20) ya Vyoo. Mradi huu unatekelezwa kwa njia ya ‘force Account’ na Fundi aitwaye MOLLO PRISON CORPORATION SOLE kwa thamani ya Tshs. 63,450,000/=
Mwenge ukiwa Laela Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alikagua Klabu ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika shule ya Sekondari Uchile ilianzishwa tarehe 18/09/2021 ikiwa na jumla ya washiriki 50 kati yao wasichana 30 na wavulana 20. Klabu hii ya UKIMWI ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana hasa wanafunzi shuleni kuhusu kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Vilevile, klabu inajihusisha na utoaji wa elimu kuhusu lishe bora kwa vijana na wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Miongoni mwa mafanikio ya klabu hii ni:- Klabu imefanikiwa kutoa elimu kuhusu Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa vijana wenzao 257 kati yao wasichana ni 138 na wavulana 119 kwa njia ya sanaa hasa nyimbo, maigizo na utoaji elimu kwa njia ya majarida, Klabu imefanikiwa kuanzisha bustani ya mboga mboga kwa ajili ya utoaji wa lishe bora shuleni.
Mwenge ukiwa Laela Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa alikagua kikundi cha New Vision Team na uwakabidhi mkopo wa Mashine ya Kutengeneza tofali za blocks yenye thamani ya shilingi 55,000,000/= (mashine ina thamani ya shilingi 30,000,000/= na mixer yake ya shilingi 9,000,000/= na mtaji wa shilingi milioni 16,000,000). Pia tunaomba ukabidhi Mikopo yenye thamani ya shilingi 50,000,000/= kwa vikundi vitano vya Wanawake, kimoja cha Vijana na Mtu mmoja mweye ulemavu. Mikopo yote ina thamani ya shilingi 105,000,000/=.
WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2022
1. Sahili Nyanzabara Geraruma
2. Rodrick Romward Ndyamukama
3. Zadida Abdalla Rashid
4. Gloria Festo Peter
5. Ali Juma Ali
6. Emmanuel Ndege Chacha
Tunashukuru miradi yetu yote imekubaliwa na kuwekwa mawe ya msingi.
Kazi iendelee
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa