• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

MAPENDEKEZO YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

Tarehe ya kuwekwa: January 17th, 2021

Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga limepitisha bajeti ya shilingi 31,545,302,988.51 leo tarehe 16/1/2021 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha kilimo katika mji mdogo wa Laela.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Nyangi John Msemakweli wakati akiwasilisha alisema “Mpango wa bajeti wa Halmashauri ya Sumbawanga kwa mwaka 2021/22, umeandaliwa kwa kuzingatia mambo muhimu yafuatayo”;

Sheria ya Bajeti Na 11 ya mwaka 2015

Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2020/21

Mpango wa Taifa wa Miaka mitano (2016/2017 – 2020/2021)

Dira ya Taifa ya 2025

Malengo 17 ya Maendeo endelevu  ya Dunia (SDGs) 2030

Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala ya mwaka 2020

Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Halmashauri (Council Strategic Plan)-2021/22-2025/26

Vipaumbele vya Halmashauri kutokana na Zoezi la Uibuaji wa Viaumbele vya Miradi ya Maendeleo lilivyofanyika kwa Kata Zote 27.

2.1 Masuala Mahsusi yaliyozingatiwa na vipaumbele 

Pamoja na miongozo ya Kitaifa na ya kisekta, masuala mahsusi yanayotokana na changamoto za utekelezaji wa bajeti iliyopita yamejumuishwa katika mpango huu ambayo ni kama ifuatavyo:

  • Utengaji wa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ambayo haijakamilika ili iweze kukamilika na kutoa matokeo tarajiwa.

Kutumia fursa ya uwepo wa wadau mbalimbali wa maendeleo katika utekelezaji wa vipaumbele vya Halmashauri.

Kuhakikisha Halmashauri inaanza kupunguza utegemezi wa serikali kuu katika kuendesha shughuli zake kwa kufanya yafuatayo;.

Ujenzi wa Stendi Mpya katika Mji mdogo wa Laela umeanza kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Maombi maalumu ya fedha Tshs 2,000,000,000 yamewasilishwa TAMISEMI kwa ajili ya kuendeleza ujenzi kwa mujibu wa mchoro.

Kuweka utaratibu wa usimamizi wa makusanyo na matumizi ya mapato/fedha zinazokusanywa ngazi ya msingi.  Zoezi hilo litaanza kipindi nusu ya pili ya mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2021.

Kutumia fursa za rasilimali zinazomilikiwa na Halmashauri katika kufanya uwekezaji

Kuimarisha timu za mapato za kata zilizoanzishwa mwaka wa fedha 2020/21 katika kusimamia ukusanyaji wa mapato.

Kuendelea na ulipaji wa malimbikizo ya madeni ya watoa huduma na Watumishi.

Upangaji sahihi wa vipaumbele katika kutekeleza malengo ya idara na Halmashauri kwa ujumla kwa kutumia rasilimali fedha inayopatikana

 

Vipaumbele vya Mpango wa 2021/22

Kwa Muhtasari Mpango na bajeti ya Halmashauri imeainisha vipaumbele vifuatavyo:

  • Uimarishaji wa mfumo na uwezo wa ukusanyaji wa mapato:
  • Mafunzo na maelekezo ya mara kwa mara kwa maafisa Watendaji juu ya sheria    zinazosimamia ukusanyaji wa mapato.
  • Kutoa huduma za ughani kwa wakulima katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ili hatimaye kuongeza mapato (kupitia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri)
  • Kuwezesha ununuzi wa mizani 10 ya mazao ya kiditali.
  • Ununuzi wa gari la kufuatilia ukusanyaji wa mapato

Kuimarisha Utawala bora na Ulinzi na Usalama

Umaliziaji wa baadhi ya  Ofisi za kata ambazo ziko katika hatua za ukamilishaji ili kuimarisha mazingira ya utoaji huduma katika ngazi ya msingi.

Kuimarisha utendaji wa mabaraza ya kata

Kuboresha huduma za kiutawala na kiutendaji:

  • Kuhakikisha stahili za wafanyakazi na wah madiwani zinalipwa ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma.

Kutoa kipaumbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) kwa ajili ya kupunguza matumizi na kuleta ufanisi katika kazi.

  • Mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Serikali za mitaa na viongozi wake wakiwemo Wenyeviti na Madiwani

Kutoa mafunzo ya utawala bora kwa viongozi wanaochaguliwa ikiwa ni wenyeviti wa vitongoji, Wenyeviti wa vijiji na Wajumbe wa Halmashauri za vijiji.

Kuimarisha utendaji wa mabaraza ya kata kwa kutoa mafunzo mbalimbali.

Kuimarisha huduma za jamii ( Afya, elimu)

  • .Kuendelea na umaliziaji wa Vituo vya Afya na Zahananti na uendelezaji wa majengo muhimu katika Hospitali ya Wilaya..
  • Kuongeza watumishi ili kukidhi mahitaji ya utoaji huduma kwa wananchi (Walimu & Watumishi wa afya)
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa na kuhakikisha upatikanaji wa  madawa na vifaa
  •   Kuendelea na utambuzi na utoaji wa huduma muhimu kwa makundi maalumu wakimemo wazee na walemavu.
  • Kufanya mafunzo watumishi wa vituo vya kutolea za Afya juu ya matumizi SBCC na MIYCAN kwa ajili ya kutathimini ukuwaji wa mtoto kwa kadi mpya za ukuwaji za WHO .
  • Kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba na vifaa vya Hospitali katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya iliyopo Mtowisa
  • Kufanya huduma mkoba za chanjo kwa kila mwezi kwa maeneo ya mbali ambayo ni magumu kufikika.
  • Ujenzi wa majengo ya Shule na usajili wa baadhi ya shule Shikizi kwa mujibu wa taratibu.
  • Ufunguzi wa shule mpya tano (5) za msingi; Mkuyuni, Taranda, Kirando, Lyanza na Kikware. Wanachi katika maeneo haya watahamasishwa kuchangia zaidi rasilmali fedha na nguvu kukamilisha mpango huo.
  • Kuendelea kusaidia ujenzi wa shule za sekondari zilizoanziswa na wananchi; Kilangawana, Ikozi, Nankhanga, Laela na Mlokola.
  • Msisitizo wa ujenzi wa shule za sekondari katika kata kumi ambazo hazina shule.

Uimarishaji na ujenzi wa miundombinu na huduma za kiuchumi.

  • Kuanzisha na kuendeleza program mbalimbali kama uanzishaji wa mashamba darasa. Mkakati huu utazihakikishia kaya usalama wa chakula na utaondoa pia tatizo la utapiamlo.

Ukarabati wa miundombinu ya mifugo kwa ajili ya kuboresha mifugo.

Kuendeleza kilimo cha kahawa na parachichi kwa ajili ya kukuza uchumi wa kaya na Halmashauri, badala ya kutegemea zaidi mazao ya asili (mahindi na Mpunga)

Kusaidia juhudi za wananchi katika kuendeleza ujenzi wa masoko ya mazao;- ambapo  vijiji vya Kinambo na Uzia vitaendelea kuwemo katika mpango huo.

Kuanza mchakato wa ujenzi wa soko la mazao kwa eneo la Ndelema (eneo limepatikana).

Kuendeleza mazao makuu manne ya mnyororo wa thamani (mahindi, mpunga, samaki na nyama). Mazao haya yako kwenye mpango wa uwekezaji wa miaka mitano kupitia mpango wa maendeleo ya Kilimo (DADP) -2021/22-2025/2026.

Kufanya upembuzi yakinifu katika masuala ya upimaji wa maumbile ardhi katika skimu ya umwagiliaji, Ilembo, Mititi na Nkwilo

Kutoa mafunzo kwa wakulima kutumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji wa zao la mpunga kwa njia ya umwagiliaji kwenye skimu za umwagiliaji.

Kutoa chanjo  kwa mifugo 250000 ya ng’ombe, kuku  na mbwa dhidi ya magonjwa ya (Ndigana kali, mdondo na kichaa cha mbwa)

Kuanzisha BMU 4 kila moja katika kata ya Nankanga, Milepa, Mtowisa na Muze

Viwanda na Biashara

Kutoa elimu ya kodi na biashara ya namna ya kuanzisha na kuendeleza biashara kwa wafanyabiashara 1500.

Kutafuta taarifa za masoko na kuzisambaza kwa wakulima na wafanyabiashara katika kata 27.

Kuhamasisha wafanyabiashara kuanzisha viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo katika kata 27

Kuendeleza sekta ya Mipango miji

           Uendelezaji wa sekta hii utachochea maendeleo-kijamii na kiuchumi na ukuaji wa sekta     ya viwanda. Mambo yafuatayo yatafanyika.

  • Kuendelea na upimaji wa maeneo kwa matumizi mbalimbali ikiwemo viwanda na makazi pamoja na urasimishaji wa makazi holela (squarter upgrading) kwa kushirikisha jamii katika maeneo husika. Upimaji wa maeneo ya taasisi kama shule na Vituo vya Afya utafanyika.
  • Kuanzisha mpango mahsusi wa upimaji ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kuendeleza upimaji katika maeneo mengine na vile vile kuwa chanzo cha mapato kwa Halmashauri.
  • Uanzishaji na uimarishaji wa stendi katika miji midogo; Kilyamatunzu, Muze na Ilemba

Kuwawezesha wananchi kiuchumi:

Kuendelea na utengaji wa asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo (ikiwa 4% wanawake, 4% vijana na 2% walemavu)

Kutenga maeneo ya wajasiliamali.

Mkazo katika maeneo Mtambukwa kwa maendeleo.

Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.

  • Huduma kwa Watoto Yatima na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
  • Kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za afya na ustawi wa Jamii (Ulinzi wa watoto nk)

Utekelezaji wa Afua za Lishe

Kutenga fedha za mapato ya ndani na zile za ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya kutekeleza Afua za Lishe.

Kushirikiana na wadau wengine ili kupanua wigo wa rasilimali na kuimarisha shughuli za Lishe

Uwekezaji katika miundominu ya taka

Msisitizo katika uwekazaji katika miundombinu ya Kata na usimamizi wa mazingira.

Kushirikisha sekta binafsi na vikundi katika suala la menejiment ya taka

Kusaidia juhudi za Wananchi katika uanzishaji na utekelezaji wa shughuli/Miradi ya maendeleo

Kutoa usaidizi kwa jamii katika kuedeleza miradi iliyoanzishwa kwa juhudi zao. Fedha maalumu  katika eneo hili

Uwekezaji

Kutumia Timu ya uwekezaji katika kuhakikisha Halmashauri inakuwa na vitega uchumi kwa ajili ya kupata mapato ya uhakika na kuondokana na utegemezi. Matarajio ni kuwa kuwekeza kupitia fursa zilizopo (Viwanja/maeneo yaliyowazi na ambayo hayajaendelezwa, majengo na mashamba/misitu)

2.2. MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2021/22

2.2.1.   Mapato

Kwa Mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri inakisia kukusanya na kupokea jumla ya Sh  31,545,302,988.51/- ambapo Shilingi 2,693,212,000/-ni mapato ya ndani na Shilingi 28,852,090,988.51/= ni ruzuku ya matumizi ya kawaida na Miradi ya maendeleo. 

Mfuko Mkuu 

Mfuko mkuu kwa mwaka wa fedha 2021/22 unakisiwa kukusanya toka vyanzo vya ndani Jumla ya Shilingi 2,693,212,000/- kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.

3.0 MATUMIZI

Mh Mwenyekiti; Matumizi ya mapato yatakayopatikana yataelekezwa katika maeneo yafuatayo:

3.1 Matumizi ya Kawaida

Matumizi ya Mapato ya Ndani:

Kwa mujibu wa mwongozo makusanyo yatakayokusanywa (mapato yasiyo-fungwa) yanatakiwa yatumike kwa mgawanyo ufuatao; asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na asilimia 60 kwa matumizi ya kawaida.

Kwa mwaka 2021/22 jumla ya Shilingi 2,693,212,000/ zinatarajiwa kukusanywa, ambapo mapato fungwa ni Shilingi 117,700,000/- na mapato mengine ni Shilingi 2,575,512,000/- 

Kwa kuzingatia mgawanyo ulioelezwa hapo juu Shilingi 1,030,204,800/- zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kiasi kingine cha shilingi  1,545,307,200./- kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Ruzuku ya Matumizi Megineyo na Mishahara

Mhe. Mwenyekiti, Serikali hutoa ruzuku kwa Halmashauri kwa ajili ya kugharamia mishahara na matumizi mengineyo kwa Idara mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri inakisia kupokea na kutumia Jumla ya Shilingi 20,371,887,000/= kwa ajili ya matumizi ya kawaida (mishahara na matumizi mengineyo). 

Matangazo

  • Baraza la Mitihani Tanzania latangaza matokeo ya darasa la saba 2024 October 29, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Orodha ya asasi zilizopata kibali cha uangalizi wa uboreshaji wa daftari mwaka 2024/2025 June 26, 2024
  • Tazama

Habari Mpya

  • Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

    September 05, 2024
  • Makabidhiano ya ofisi

    August 21, 2024
  • CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

    July 25, 2024
  • Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa

    May 25, 2024
  • Tazama

Video

Kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 0754634811

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa