Siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyoadhimishwa leo tarehe 16/06/2022 katika viwanja vya Shule ya msingi Mtowisa, kijiji cha mtowisa kilichopo kata ya mtowisa mgeni rasmi akiwa ni Mh.Sebastian Waryuba Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga.
Mgeni rasmi alichukua nafasi hiyo kuongelea mambo yafuatayo ya kijamii.
Kulisihi dawati la jinsia kufanya kazi kwa weledi ili kupunguza au kuondoa kabisa mimba za utotoni ikiambatana na unyanyasaji wa watoto.
Kuhamasisha ulinzi na usalama katika Halmashauri na sehem zote ili kuondoa matendo yoyote yanayoweza pelekea kunyanyaswa kwa mtoto.
Pamoja na hayo pia alihamasisha umati ulioshiriki maadhimisho hayo kutunza chakula ili kuepukana na njaa hii ni kutokana na uzalishaji wa mazao mwaka huu usio ridhisha ambao umesababishwa na kutokuwepo na mvua za kutosha.
Pia aliongelea na kusisitiza watu kujiandaa kuhesabiwa na kuendelea kutoa elim ili watu wote wawe na utayali huo maana mnamo tarehe 23/08/2022 ni tarehe ambayo sensa ya watu na makaazi itakapohesabiwa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa