Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga likiongozwa na Mwenyekiti Mh. Gerald Kalolo Ntila na Katibu wake Bi. Lightness Msemo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri, limeendesha vikao kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 27/5/2022 na kuhitimishwa tarehe 28/5/2022 katika ukumbi wa chuo cha kilimo Laela.
Kwa siku ya tarehe 27/5/2022 Baraza hilo limepokea taarifa zilizowasilishwa na Madiwani wa kila kata ambazo zilihusu mambo mbalimbali kama vile miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata, mwenendo wa mavuno ya mazao ya kilimo, shughuli za ufugaji, hali ya usalama, idadi ya watu na idadi ya watumishi waliopo katika idara ya mbalimbali.
Aidha kwa siku ya tarehe 28/5/2022, Baraza lilipokea taarifa ya mapato na matumizi iliyowasilishwa na Mweka Hazina Ndg. Itendele Limbe Maduhu kwa niaba ya Mkurugenzi, Mweka Hazina alisema kuwa “Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilikisia kukusanya mapato ya ndani na kupokea fedha toka kwa Wahisani na Serikali Kuu jumla ya Tsh 40,424,734,297.00 kwa mchanganuo ufuatao;-
A: MAPATO.
Mhe. Mwenyekiti,
Kwa kipindi cha Mwezi Marchi 2022 Halmashauri imefanikiwa kukusanya na kupokea jumla ya TZS 2,101,846,408.48 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.
Kati ya fedha hizo makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani ni kiasi cha TZS 161,184,082.00 sawa na asilimia 92 ya bajeti ya makusanyo kwa mwezi Machi 2022 ambapo ilipanga kukusanywa kiasi cha TZS 175,912,257.00 kutoka kwenye mapato ya ndani.
Pamoja na makusanyo ya mapato ya ndani pia Halmashauri imepata fedha kutoka Serikali Kuu kwa mchanganuo ufuatao:
Ruzuku ya Mishahara ni TZS 1,639,488,330.00 sawa na asilimia 7 ya bajeti ya mwaka Matumizi Mengineyo (OC ) ni TZS 25,706,583.33 sawa na asilimia 1 na Fedha za Miradi ya Maendeleo ni kiasi cha TZS 275,467,413.15sawa na asilimia 3
Makusanyo hayo ya mwezi Machi 2022 yamepelekea kuwa na jumla ya makusanyo ya kiasi cha TZS 25,107,741,648.73kwa kipindi cha Julai –Machi 2022 sawa na asilimia 62 kwa mchanganuo ufuatao;-
Kati ya makusanyo ya kiasi cha TZS TZS 1,890,374,187.76 yatokanayo na mapato ya ndani, kiasi cha TZS 69,749,121.47 ni mapato fungwa (CHF, PAPO KWA PAPO NA ADA SHULE ZA SEKONDARI) na kiasi cha TZS 1,820,625,066.29 ni mapato yasiyofungwa (Mapato Halisi).”
Mbali na taarifa ya mapato, Mweka Hazina aliwasilisha taarifa ya matumizi, alisema kuwa “ Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri iliidhinishiwa kutumia jumla ya TZS 40,424,734,297 kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani, Wahisani na Ruzuku toka Serikali Kuu.
Kwa kipindi cha Mwezi Machi 2022,Halmashauri imetumia jumla ya TZS2,397,278,321.00 sawa na asilimia 06 ya lengo la matumizi kwa mwaka kwa mchanganuo ufuatao;-
Matumizi hayo yanapelekea Halmashauri kutumia kiasi cha TZS 23,301,729,334 kwa kipindi cha Julai – Machi 2022 sawa na asilimia 58.
Mchanganuo wa matumizi ya kuanzia Julai – Machi 2022 ni kama ifuatavyo:
Mbali na taarifa ya mapato na matumizi, iliwasilishwa taarifa ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Afisa Mipango kwa niaba Mkurugenzi, alisema “Kwa mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga iliandaa mpango wa Maendeleo unaojumuisha mahitaji ya vipaumbele vya wananchi kama vilivyoibuliwa kupitia Mpango wa fursa na vikwazo kwa Maendeleo (O&OD). Wakati wa mchakato huo, Mipango na Bajeti za miradi ya vipaumbele iliombewa fedha kutoka Halmashauri, Serikali kuu, Mashirika ya kijamii, na Asasi zisizokuwa za kiserikali, aidha baadhi ya miradi ya maendeleo imeendelea kutegemea nguvu za Wananchi.
BAJETI YA MIRADI ILIYOIDHINISHWA
Kwa mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri iliidhinishiwa kupokea na kutumia Fedha za maendeleo jumla ya Tsh. 12,426,554,000/=, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kati ya Fedha hizo, fedha za ndani (Local fund Serikali kuu) ni Tsh 4,385,713,000/= sawa na 35.3%, fedha za nje (Foreign fund) ni Tsh 6,996,641,000.00 /= sawa na 56.3% na Fedha za Miradi ya makusanyo ya mapato ya ndani (Own source) ni 1,044,200,000.00/= sawa na asilimi 8.4 ya Bajeti yote ya Maendeleo ya Halmashauri.
MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO
Hadi kufikia tarehe 31, Machi 2021/22, Halmashauri imepokea na kukusanya fedha za miradi ya Maendeleo Tsh. 9,724,369,411/- sawa na asilimia 78 ya fedha za Miradi kati ya kiasi hicho Tsh 4,405,130,330.79 ni mapokezi nje ya ukomo wa bajeti sawa na asilimia 47 ya mapokezi ya fedha za Miradi. Halmashauri imetumia Jumla ya Tsh. 5,028,478,822/- sawa na asilimia 52 ya mapokezi”
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa