Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga likiongozwa na Mwenyekiti Mh. Gerald Kalolo Ntila na Katibu wake Bi. Lightness Msemo ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri, limeendesha vikao katika ukumbi wa chuo cha kilimo Laela.
Aidha Baraza lilipokea taarifa ya mapato na matumizi iliyowasilishwa na Mweka Hazina Ndg. Itendele Limbe Maduhu kwa niaba ya Mkurugenzi, Mweka Hazina alisema kuwa “Kwa mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri inakisia kukusanya na kupokea fedha jumla ya Sh. 36,396,350,000 ikiwa ni pungufu kwa 1% ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2021/2022 ya shilingi 36,841,139,380. Katika fedha hizo, Shilingi 3,961,881,000 ni mapato ya ndani, shilingi 21,464,066,000 ni ruzuku ya mishahara, shilingi 10,046,547,000 ni fedha za miradi ya maendeleo na shilingi 923,856,000 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida.
MAPATO YA NDANI
Kwa Mwaka wa fedha 2023/24 Halmashauri inakisia kukusanya fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato ya ndani kiasi cha Shilingi 3,961,881,000 /- ambapo kati ya Kiasi hicho Shilingi 3,699,701,000.00 ni fedha kutoka Mapato yasiyofungwa na Shilingi 262,180,000- ni fedha za Mapato fungwa.
RUZUKU YA SERIKALI KUU NA FEDHA ZA NJE
Halmashauri inategemea kupokea Shillingi 32,434,469,000/= ikiwa ni ruzuku ya uendeshaji wa shughuli za Utawala kwa idara mbalimbali, Mishahara pamoja na Miradi ya Maendeleo.
MATUMIZI
Matumizi ya mapato yatakayopatikana kama ilivyokisiwa yataelekezwa katika maeneo yafuatayo:
MATUMIZI YA KAWAIDA
Matumizi ya Mapato ya Ndani:
Kwa mujibu wa mwongozo makusanyo yatakayokusanywa (mapato yasiyo-fungwa) yanatakiwa yatumike kwa mgawanyo ufuatao; asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na asilimia 60 kwa matumizi ya kawaida.
Kwa mwaka 2023/24 jumla ya Shilingi 3,937,061,000 yanatarajiwa kukusanywa, ambapo mapato fungwa ni Shilingi 262,180,000 na mapato mengine yasiyofungwa ni Shilingi 3,674,881,000
Kati ya fedha zitakazokusanywa Shilingi 1,469,952,400 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na kiasi kingine cha Shilingi 2,204,928,600 kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni maelekezo ya kutumia 40% ya fedha za Mapato ya ndani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na 60% kwa ajili ya Matumizi mengineyo kwa mujibu wa Mwongozo wa Bajeti ya Mwaka 2023/2024 nje ya Mapato fungwa.
Ruzuku ya Matumizi Megineyo na Mishahara
Serikali hutoa ruzuku kwa Halmashauri kwa ajili ya kugharamia mishahara na matumizi mengineyo kwa Idara mbalimbali. Kwa mwaka wa fedha 2023/24, Halmashauri inakisia kupokea na kutumia Jumla ya Shilingi 21,464,066,000/- kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
SEKTA YA ELIMU
Likizo za walimu 205,660,000
Gharama za Uhamisho 116,601,000
MIRADI YA MAENDELEO
Kwa mwaka 2023/24 Halmashauri inategemea kupokea na kutumia Jumla ya Tshs. 11,516,499,400.00- kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo, kati ya fedha hizi Tsh 5,039,110,000 - ni Ruzuku ya Miradi toka Serikali kuu na Tsh 5,007,437,000/= ni fedha za wafadhili na Shilingi 1,469,952,400 ni mchango wa mapato ya Ndani ya halmashauri katika utekelezaji wa Miradi. Mchanganuo wa miradi umeambatishwa (rejea kiambata B)
Jedwali Na. 15: MAKISIO YA MIRADI YA MAENDELEO KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA MWAKA 2023-2024
NA.
|
IDARA
|
JINA LA MRADI
|
BAJETI TENGWA
|
MAPATO YA NDANI
|
|||
1
|
BIASHARA
|
Ujenzi wa kiwanda cha matofali kata ya Kilyamatundu
|
273,700,000 |
|
|
Ukarabati wa ukumbi wa biashara na kuweka samani
|
30,000,000.00 |
|
|
Ujenzi wa miundombinu ya stendi ya Mtowisa
|
70,000,000.00 |
2
|
UTAWALA NA UTUMISHI
|
Ukamilishaji wa Ofisi ya Kata ya Lusaka
|
25,000,000.00 |
3
|
MAENDELEO YA JAMII
|
Kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi
|
367,488,100 |
4
|
MALIASILI
|
Kupanda miti katika shamba la Makuzani
|
25,000,000.00 |
5
|
MAZINGIRA NA TAKANGUMU
|
Kutenga eneo la dampo na kulijenga
|
20,000,000.00 |
6
|
AFYA
|
Ukamilishaji wa kituo cha afya kata ya Muze
|
400,000,000 |
1
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kuwezesha kuweka mipaka kwenye eneo la umwagiliaji skimu ya umwagiliaji sakalilo 6500ha na ilemba 1,650ha ifikapo juni 2024
|
3,700,000 |
2
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kufanya upembuzi yakinifu katika masuala ya upimaji wa maumbile ardhi katika Skimu za umwagiliaji katika kata za Kaoze, kilangawana, kipeta, mpui na kaengesa ifikapo Juni, 2024.
|
25,000,000 |
3
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kuwezesha Kurasimisha eneo la uwekezaji kwaajili ya ujezi wa soko, viwanda na maghala katika kijiji cha Kipeta ifikapo juni 2024
|
18,632,000 |
4
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora za mihogo kwa eneo la ekari moja kwa wakulima 13 wa 13 za bonde la Ziwa Rukwa ifikapo Juni 2024
|
7,500,000 |
5
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kukamilisha ujenzi wa soko moja katika Kijiji cha Kinambo ifikapo Juni 2024
|
25,000,000 |
6
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kununua zeti nne za mashine za kubangua korosho kwa ajili ya kata 4 za Muze, Mtowisa, Zimba na Kaoze ifikapo Juni 2024
|
3,500,000 |
7
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kuanzisha mashamba darasa ya mahindi, mpunga ngano na alizeti katika kata 27 za Halmashauri ifikapo Juni 2024
|
8,900,000 |
8
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kununua miche 2,000 iliyoboreshwa ya parachichi (hasi) na kuisambaza katika Kata nane za Laela, Mpui, Kaengesa, Milepa, Muze, Mtowisa, Ilemba na Kipeta ifikapo Juni, 2023
|
8,000,000 |
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kukamilisha mahitaji ya maghala manne ya Kaoze, Sakalalo, Mtowisa na Muze na kuyasajili kwa ajili ya kuhifadhia mazao na pembejeo za kilimo ifikapo juni 2024
|
13,000,000 |
9
|
KILIMO, MIFUGO NA UVUVI
|
Kununua kilo 500 za mbegu za korosho na kuzigawa kwa wakulima wa Kata 13 za Bonde la Ziwa Rukwa ifikapo juni 2024
|
5,167,000 |
10
|
MIFUGO NA UVUVI
|
Kukamilisha ujenzi wa nyumba ya afisa ugani Sandulula ifikapo juni 2024
|
19,000,000 |
11
|
MIFUGO NA UVUVI
|
Kujenga machinjio moja ya ng’ombe katika kijiji cha Kilyamatundu ifikapo juni 2024
|
21,000,000 |
7
|
ELIMUMSINGI
|
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule za Rukwa (1) na Kituku (1)
|
40,000,000 |
8
|
ELIMU SEKONDARI
|
Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule za Lula na Kilangawana
|
40,000,000 |
|
MAENDELEO YA MIUNDOMBINU YA VIJIJI NA MIJI
|
Fidia ya eneo la stendi laela
|
20,365,300 |
|
JUMLA
|
|
1,469,952,400.00 |
MIRADI YA KIMKAKATI:
Pamoja na miradi inayoombewa fedha, kuna miradi maalumu ambayo itaendelea kuombewa na kuongezewa nguvu kazi ya utalaamu na rasilimali fedha kwa ajili ya kupata takwimu sahihi (baseline data) na maandiko yanayokidhi vigezo vya kitaalam ili kuendelea kuongeza pato la Halmashauri katika kuhudumia wananchi wake sambamba na kupunguza utegemezi wa fedha kutoka serikali kuu. Miradi hiyo ni kama inavyoonekana katika Jedwali lifuatalo:-
MIRADI YA KIMKAKATI
NA
|
MRADI
|
01
|
Ujenzi wa soko na maghala ya kuhifadhia mazao katika kijiji cha Kilyamatundu
|
02
|
Ujenzi wa Soko la Mazao na maghala ya kuhifadhia mazao katika kijiji cha Ndelema
|
03
|
Uanzishaji wa ujenzi wa shule ya English Medium
|
04
|
Uanzishaji wa mwalo wa Nankanga (Sofia Town)
|
VIHATARISHI/CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2023/2024
Pamoja na mapendekezo yaliyotolewa, kuna maeneo ambayo yanaweza kuathiri utoaji wa huduma na kuwa kinyume cha mategemeo ya mpango huu. Miongoni mwa changamoto ni kama ifuatavyo:-
Ukomo wa bajeti uliotolewa kwa maeneo mbalimbali:
Kutokana na mwongozo wa uendeshaji wa mitihani ya upimaji wa kidato cha pili (FTNA) mtihani wa kidato cha nne (CSEE) na kidato cha sita (ACSEE), Ukomo wa bajeti uliotolewa kwa ajili ya upimaji wa kidato cha pili (FTNA), kidato cha nne (CSEE) na kidato cha sita (ACSEE) ni mdogo ikilinganishwa na hali halisi.
ii. Majanga ya Asili na Hali ya hewa
Uwepo uwezekano wa janga la kimbunga, milipuko ya Magonjwa kama vile kipindupindu na corona inaweza kuwa na athari kwa wananchi katika uzajilishaji mali na tija, hivyo kuathiri shughuli nyingine zinazotegemewa kuchangia pato la Halmashauri zikiwemo leseni za Biashara, Mifugo na Uvuvi.
Katika Bajeti ya Mwaka 2023/2024 Halmashauri inategemea kukusanya fedha za Mapato ya ndani kutokana na Mazao kwa 62% sawa na Shilingi 2,079,075,000 changamoto zozote za kipato duni kwa wakulima au ukosefu wa masoko na hivyo kuathiri bei za Mazao zitakuwa na athari za moja kwa moja katika ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na hivyo kuathiri utekelezaji wa Bajeti.
Uwepo wa Defaulters na Wakwepa kodi
Halmashauri imekuwa ikipitia changamoto ya defaulters kutokana na Jiografia yake sambamba na uhaba wa taasisi za kifedha kila Kijiji ambako ndio chimbuko la ukusanyaji wa Mapato, aidha changamoto ya utoroshaji Mazao kwa njia za vyombo vya Usafiri vya Serikali, Magari binafsi, Mabasi madogo na makubwa ndani ya magari (viti vya abiria) iwapo nguvu kazi na udhibiti mdogo ukitokea unaweza athiri bajeti ya Halmashauri.
Upungufu wa watumishi katika kada za Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Ukusanyaji wa Mapato
Halmashauri inalo tatizo la upungufu mkubwa katika baadhi ya idara zenye mchango wa moja kwa moja katika usimamizi wa Miradi na Mapato ya ndani zikiwemo kada za Ujenzi, Manunuzi, Uhasibu na Maendeleo ya Jamii hadi ngazi za chini wakiwemo pia Watendaji wa Kata na Vijiji.
Hatua za kukabiliana na changamoto
Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Ukusanyaji wa Mapato
UMBILE LA BAJETI YA HALMASHAURI KWA MWAKA 2023/2024
NA
|
MAPATO
|
KIASI (TSHS)
|
A
|
Mapato yatokanayo na Ruzuku
|
|
Ruzuku ya Mishahara (PE)
|
21,464,066,000 |
|
Mapato Mengineyo (OC)
|
923,856,000 |
|
Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo (DEV)
|
10,046,547,000 |
|
Jumla ndogo
|
32,434,469,000 |
|
2
|
Mapato yatokanayo na vyanzo vya Ndani
|
|
|
Mapato ya Ndani
|
3,961,881,000 |
|
JUMLA KUU(MAPATO)
|
36,396,350,000 |
B
|
MATUMIZI
|
|
1
|
Matumizi yatokanayo na vyanzo vya Ndani (Own source)
|
|
Mishahara (PE)
|
0 |
|
Matumizi Mengineyo (OC)-
|
2,219,820,600 |
|
Jumla ndogo
|
2,219,820,600 |
|
2
|
Matumizi yatokanayo na Ruzuku
|
|
Ruzuku ya Mishahara (PE)
|
21,464,066,000 |
|
Mapato Mengineyo (OC)
|
923,856,000 |
|
Jumla ndogo
|
22,387,922,000 |
|
3
|
Miradi ya Maendeleo
|
|
Ruzuku ya Maendeleo
|
10,046,547,000 |
|
Miradi ya Maendeleo kwa vyanzo vya ndani vya Halmashauri(Own Source)
|
1,479,880,400 |
|
Mapato Lindwa
|
262,280,000 |
|
Jumla ndogo (Miradi)
|
11,526,427,400 |
|
|
JUMLA KUU (Matumizi)
|
36,396,350,000 |
HITIMISHO
Kwa heshima na taadhima, naomba sasa kuwasilisha taarifa hii ya Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2023/2024 yenye jumla ya Shilingi 36,396,350,000
Naomba kuwasilisha.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa