Leo Tarehe 20/08/2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Bi. Lightness S. Msemo, Diwani wa kata ya Laela Mh. James Mwanilyela, OCD Ndugu J.Ntandu pamoja na watalam toka ofisi ya Mkurugenzi wamefanya kikao cha ndani na wenyeviti wa mitaa,wafanya biashara hususani wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na wafanyakazi wao pamoja na wafanyabiashara wa chakula wa mji mdogo wa Laela. Lengo la kikao hicho ilikuwa ni mwendelezo wa hamasa za sensa, maandalizi ya Mwenge na kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Miongoni mwa mambo yaliyo ongelewa mbali na kutatua matatizo yanayo wakabili wafanya biashara hao ni kama yafuatayo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga alisisitiza kuwepo na ushirikiano baina ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni na wafanyakazi toka ofisini kwake pamoja na wafanyakazi toka ofisi ya OCD lengo ni kuendelea kuboresha usalama wa maeneo ya mji mdogo wa Laela na viunga vyake.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga alisisitiza pia swala la uwepo wa gonjwa la UVICO 19 na kuwasihi wafanyabiashara hao kuzingatia usafi kwa kuweka ndoo ya maji na vitakasa mikono kwa ajili ya wateja wao waingiapo na watokapo waweze kunawa mikono.
Jambo lingine lililo ongelewa ni elimu ya mlipa kodi, Afisa biashara wa Halmashauri ya Sumbawanga Mama Veronica Mwandiga alitoa elimu juu ya kulipa kodi ya huduma (Service levy) pamoja na kuwasihi wafanya biashara kulipa kodi zao kwa wakati ili kuepusha usumbufu baina yao.
Pia aliongelea suala la uwepo wa daftari la wageni na kuwasihi wahudumu wa nyumba za kulala wageni wahakikishe wanasimamia kikamilifu wateja wao kujiandikisha kwenye daftari hilo, sio tu kwa usalama bali pia ili kuweza kusaidia kiwango sahihi cha kodi kinacholipwa na wamiliki wa nyumba hizo za kulala wageni.
Mganga mkuu wa wilaya Ndugu Y.Msuya nae alisisitiza swala la usafi, kwa upande wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni alisisitiza uwepo wa usafi ndani na nje ya vumba ili kuepusha magonjwa kama vile magonjwa ya ngozi hasa kama mashuka hayatasafishwa na kunyooshwa vizuri kabla ya kutumiwa.
Upande wa wafanyabiashara wa chakula Mganga mkuu aliwasihi pia waweke maji ya moto ya kunawa wateja wao pia kuhakikisha vyakula vina andaliwa katika mazingira safi na salama ili kuepusha magonjwa ya mlipuko hususani kuumwa matumbo na pia itasaidia kupunguza kusambaa kwa UVICO 19.
OCD nae alipata wasaa wa kutoa neno kwa wafanyabiashara hao hasa wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni, OCD Ndugu J.Ntandu alisisitiza uwepo wa usalama na kama endapo itatokea mteja analeta usumbufu kwa wahudumu wa nyumba hizo za kulala wageni au kama hawajulikani walikotokea na hawataki kutoa ushirikiano basi wahudumu wasisite kutoa taarifa kwake ili kuendelea kudumisha amani katika eneo la mji mdogo wa Laela viunga vyake.
Bila kusahau swala la sensa viongozi wote kwa pamoja walisisitiza kila mmoja kuwa barozi wa kuhamasisha watu wajitokeze ili kuhesabiwa kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
Mwisho wafanyabiashara wali ishukuru ofisi ya Mkurugenzi pamona na ofisi ya OCD kwa kuwakutanisha kwa mala ya kwanza ili kuweza kutatua matatizo wanayo kutana nayo, kupata elimu mbalimbali toka kwa watalam na kuahidi kutoa ushirikiano kwa yote yaliyoagizwa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa