Kamati ya Siasa Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Ndg. Chrisant J. Kalasa imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Miradi iliyotembelewa na maoni ya kamati hiyo katika kila mradi ni kama ifuatavyo:-
1. Shule ya Sekondari Kalumbaleza
Wajumbe warifurahi juu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Kwa kujenga shule nzuri ya Sekondari na imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kutupatia fedha pia. Shule hiyo imekamilika na inatumika kwa sasa.
2. Ujenzi wa vyumba 3 vya Madarasa Shule ya MSINGI Mukamanye.
Kamati imefurahishwa na usimamizi na ubora wa Mradi huo. Kamati ilipongeza uliongozwa Kata akiwemo Mhe. Diwani kwa ushirikiano na kushirikisha Jamii ipasavyo na kusababisha kuchangia nguvu zao kikamilifu, ambazo zimesababisha kukamilika Kwa mradi na kubaki na Salio.
3. Zimba - Ujenzi wa vyumba 3 vya Madarasa Shule ya Sekondari
Kamati haijaridhishwa na maendeleo ya Ujenzi kwani Kasi ya Ujenzi siyo nzuri. Pia Kamati ilibaini Kuna ushirikiano dhahifu baina ya viongozi wa Kata hivyo kushindwa kushirikisha Jamii katika utekelezaji wa Mradi.
Chama kimeshauri ili kuhakikisha Mradi huu unakamilika tuombe Kampuni ya Helleumnobal Gas kusaidia nguvu za Wananchi.Kamati imeahidi kurejea tena Zimba kuona Kasi ya Ujenzi.
4. Kutembelea kikundi Vijana Bodaboda Sakalilo.
Kamati ya SIASA WILAYA imeipongeza Halmashauri Kwa kuwezesha kikundi hicho na kukikopesha Tsh 7,000,000/-. Aidha kikundi kimepongezwa Kwa jinsi kinavyofanya kazi na kufanikisha kurejesha fedha kiasi Cha Tsh 6,000,000/- Hadi Sasa.
Kamati imeshauri kuwa Halmashuri iwape kipaumbele kingine wakati wa utoaji wa mikopo ili kuimarisha Mtaji wao.
Halmashuri imeshauriwa kuongeza mkakati wa ukusanyaji wa madeni yote katika Vikundi vilivyokopeshwa.
5. Ujenzi wa Zahanati Liwelyamvula
Kamati ya siasa wilaya imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kutoa kiasi cha shilingi Milion miamoja (100,000,000) ili kuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo. Pia kamati imefurahishwa na mwamko mzuri wa wananchi katika kushiriki ujenzi kwa kuchimba msingi na kukusanya mawe.
Pia ilipongeza Halmashauri Kwa kuafiki Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji hicho. Kamati imeitaka Halmashuri kuhakikisha Mradi unasimamiwa Kwa karibu ili kuepusha mapungufu yanayoweza kujitokeza. Imeitaka Halmashauri kuhakikisha Mradi unakamilika kabla ya kuanza Kwa msimu wa Mvu,
6).Ujenzi wa vyumba 3 vya Madarasa Shule ya msingi Kipeta.
Kamati haikuridhishwa na usimamizi wa Mradi Kwa jumla baada ya kubaini mapungufu mbali mbali yakiwemo, kuanza kupasuka Kwa Sakafu, namna ya upauaji na uandaaji wa taarifa juu ya ushiriki wa mchango wa Wananchi
Kamati imeshauri mambo yafuatayo yafanyike Halmashauri ione namna ya uwekaji wa maru maru katika vyumba vya Madarasa, pia taarifa ya Mradi iandaliwe upya na iwasilishwe Ofisi ya Chama ikionesha mchanganuo wa gharama sahihi wa nguvu za Wananchi.
7). - Ujenzi wa vyumba vine vya madarasa shule ya sekondari Mnokola
Mradi wa ujenzi wa madarasahayo upo hatua za mwisho kamati ya Siasa Wilaya ilishauri kuwa Halmashuri ihakikishe Mradi unakamilika na unaanza kutoa huduma stahiki Kwa jamii ili kuondoa usumbufu wanaoupata wanafunzi wa kata hiy .
8). Ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa
Kamati ya Siasa Wilaya ilipongeza Serikali kujenga shule hiyo katika eneo la mji mdogo wa Laela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga maana itapelekea mji huo kukua kwa haraka.
Kamati ilishauri Ujenzi wa jiko la dharula ifanyike mapema. Pia Kisima Cha maji kichimbwe mapema, ambapo Mkuu wa Wilaya alimuagiza Meneja wa RUWASA kuhakikisha na kuchimba kisima hicho Kwa kutumia mitambo ya Mkoa.
9).Ukarabati wa Vyumba 6 vya madarasa shule ya sekondari Mpui.
Ukarabati unaendelea vizuri kwa ubora wa hali ya juu. Kamati ya Siasa Wilaya imeshauri kuwa usimamizi wa karibu uongezeke ili ukarabati huo ukamilike kwa ubora. Katika ukarabati huo Halmashauri imetoa kiasi cha shiringi 50,000,000 kamati ya Siasa Wilaya imeshauri Halmashauri kuongeza Kiasi cha shiringi 28,000,000 ili kukamilisha vyumba hivyo.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa