Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kalolo Ntila ameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuichagua Halmashauri yake kuwa miongoni mwa Halmashauri chache zilizobahatika kupata mradi wa lishe endelevu. Mradi huu unatekelezwa kwa muda wa miaka minne kwa mikoa mitano ambayo ni Dodoma, Morogoro, Iringa pamoja na Rukwa. Kwa mkoa wa Rukwa Halmashauri zote zimebahatika kupata mradi huu.
Mh. Mwenyekiti ameitaka kamati ya lishe kupitia mradi iiwezeshe jamii kutambua wapi inakosea kwa sababu Halmashauri yetu ina chakula cha kutosha pia ina matunda mengi na mifugo mingi lakini imekuwa na asilimia kubwa ya utapia mlo tofauti na matarajio ya wengi.
Aliwaomba viongozi wa dini ambao pia ni wajumbe wa kamati ya lishe kufikisha elimu ya kutosha kwa waumini wao kuhusu suala zima la lishe kwani waumini wamejenga imani kubwa kwa viongozi wao kiasi kwamba ujumbe utafika mapema na utekelezaji utakuwa rahisi.
Mwenyekiti alisema “natamani kuona Halmashauri yangu inakuwa ya kwanza kwa mkoa wa Rukwa katika kutekeleza mradi huu kwa kuhakikisha tunaweka historia ya kupunguza utapia mlo kwa asilimia kubwa kama sio kutokomeza kabiasa”.
Matarajio ya mradi ni baada ya miaka minne kuona afya iliyoboreka kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa na watoto chini ya miaka mitano pia kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na afya bora ili aweze kuchangia ukuaji wa pato la taifa.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa