Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mara ya kwanza imefanya kikao cha baraza lake la madiwani kwenye makao makuu mapya yaliyopo katika Mamlaka ya mji mdogo Laela. Kikao hicho kilifanyika siku ya Alhamisi tarehe 21/11/2019 katika ukumbi wa Chuo cha Kilimo Laela.
Akiongea katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake alioutoa wa kuhamishia makao makuu ya Halmashauri kutoka Manispaa ya Sumbawanga na kuyapeleka kwenye mamlaka ya mji Mdogo wa Laela. Alisema dhamira ya Mh. Rais ni kuhakikisha huduma zinasogezwa kwa wananchi na haipaswi makao makuu ya Halmashauri mbili kuwa ndani ya Halmashauri moja.
Pia alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ndugu Nyangi John Msemakweli kwa kutekeleza agizo la Mh. Rais la kuahamia katika makao makuu mapya ndani ya siku 14 kama alivyo ahidi mbele ya Mh. Rais. Alisema jambo hilo lilikuwa ni gumu sana lakini Mkurugenzi amehakikisha jambo hilo limetekelezwa kama alivyoagizwa. Vile vile aliwapongeza watumishi ambao wamekwenda kuanza makazi mapya kwa kipindi cha muda mfupi bila kuathiri utendeaji wao wa kazi.
Pamoja na mambo mengine pia Mh. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri alizungumzia suala la baadhi ya Kata kuwa ziko umbali mrefu zaidi ya kilometa 150 kutoka makao makuu ya Halmashauri hiyo. alitaja kata hizo ambazo ni Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui, na Mtowisa. Alisema kuna kila sababu ya kutazama ni kwa namna gani wananchi wa maeneo hayo wanaweza kusaidiwa kupata huduma kwa ukaribu.
Baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Wah. Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kuweza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 6, Oktoba 2019 alipokuwa katika ziara yake ya siku 3 ndani ya Mkoa wa Rukwa ambapo aliiagiza halmashauri hiyo kuhamia Laela.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa