Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 yenye thamani ya shilingi 33,481,657,980/= katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga tarehe 26/01/2019.
Aidha katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Kalolo Ntilla alisema maeneo ya vipaumbele ni uanzishwaji wa miradi ya maendeleo ambayo ni pamoja na ujenzi wa stendi katika kata za Mtowisa, Kilyamatundu, Ilemba na mji mdogo wa Laela.
Katika bajeti ya mwaka 2018/2019 Halmashauri imefanikiwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari na msingi, uanzishwaji wa shule mbili za sekondari za Kipeta na Lula, ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la walimu Kwela Sekondari (six in one), ukarabati wa miundombinu (madarasa, vyoo na bafu) Vuma sekondari. Aidha shule mbalimbali zimepatiwa vifaa kama bati na saruji ili kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza.
Kwa upande wa afya, Halmashauri imefanikiwa kuendeleza ujenzi wa kituo cha afya Milepa, ujenzi wa hospitali ya Wilaya Mtowisa na upatikanaji wa madawa na vifaa tiba na vitenganishi kutoka asilimia 80 hadi 98 kutokana na ongezeko la bajeti. Onezeko la vituo vinavyotoa huduma za upasuaji wa dharura kutoka vituo 2 hadi 3.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri alizungumzia uharibifu wa barabara unaosababishwa na mifugo. Alisema wananchi wapewe elimu ya kutosha ili wasilime wala kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dr. khalfany Haule alisisitiza suala la vitambulisho vya wajasilia mali kwa kuwa vinamsaidia mjasiliamali kutambulika, kupata mkopo kiurahisi, kinatumika mahali popote ndani ya nchi pia kinamsaidia mjasiliamali asiweza kulipa kodi ya aina yoyote.
Ndugu Albinus Mugonya ambaye ni Afisa Serikali za Mitaa Mkoa alialikwa kwenye kikao hicho na alizungumzia suala la wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu Halmashauri ihahikishe wanalipoti kwa wakati pia alizungumzia suala la kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha asilimia 10 za wanawake, vijana na walemavu ziendelee kutolewa kwa wakati.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa