Friday 9th, May 2025
@
Historia siku ya mtoto wa Afrika
Siku ya mtoto wa Afrika ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipok elewa na mikono isiyo na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi ambao hawakuwa na silaha,idadi halisi ya waliouwawa haijulikani lakini inakadiliwa ni watoto 176 mpaka 700.
Hector Pieterson 13 anayejulikana kama ishala ya waandamanaji (The Symbol of the Protest) alikuwa ni mmoja wa watoto wa shule aliyepigwa risasi na askari,alikimbizwa kwenye Dispensari ya kijiji na kujulikana alifariki mda mfupi baada ya kupigwa risasi. Alipopigwa risasi Hector alibebwa na Mbuyisa Makhubo 18 akisaidiana na dada yake Hector aliyeitwa Antoinette 17,walikimbilia gari la mpiga picha Sam Nzima ambaye aliwapiga picha.
Hata leo imekuwa ni picha ya kumbukumbu(Iconic image) ya machafuko hayo.Siku ya kumbukumbu na jumba la maonyesho ya Hector Pieterson yalizinduliwa juni 16,2002
“Watu wangu, leo nipo huru kwa kuwa sitosahaulika kabisa, siku itatimia ambapo kila mmoja wetu atakuwa huru, huru kutokana na unyanyasaji, huru kutokana na woga,huru kutokana na kuuwawa,nyinyi ni vijana wadogo mtaishi hadi kujiona siku hiyo na hata kama sintofanikiwa kuiona siku hiyo ninyi mnatakiwa kusadiki tu mimi nitakuwepo siku hiyo,hapa ni nyumbani kwangu pahala pa kuishi.”
Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sarafina katika filamu iliyoigiza mauaji hayo ya juni 16,1976 huko Soweto.Inaaminika kuwa maandamano hayo yaliyofanyika miaka 41 iliyopita yalikuwa mwanzo wa kuangusha utawala wa kibaguzi nchini humo.
Juni 16,ilitangazwa rasmi mwaka 1991 na Jumuiya ya Umoja wa Afrika kuwa siku ya mtoto wa Afrika.Siku hii inatoa nafasi kwa wadau wote wa haki za watoto,zikiwamo serikali mbalimbali,mashirika yasiyo ya kiserikali na hata jumuia za kimataifa kuyatazama kwa kina matatizo yote yanayowakabili watoto katika bara letu la Afrika.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa