Saturday 23rd, November 2024
@Uwanja wa Mandela
Mei Mosi ni siku ya Wafanyakazi Duniani; siku ya mshikamano na wafanyakazikatika kusimamia na kuunga mkono haki, wajibu na dhamana ya wafanyakazi katikamchakato wa maendeleo endelevu! Kazi ni utimilifu wa utu na heshima yabinadamu. Kazi inapaswa kupewa hadhi yake inayofumbatwa katika ubinadamu. Hapakuna haja ya kuwepo na ushirikiano wa dhati kati ya shule na fursa za ajirasanjari na uwiano bora wa maendeleo katika nchi. Elimu na Kazi ni chanda napete, mambo yanayotegemeana na kukamilishana, ili kuweza kupata ufanisi bora,tija na maendeleo ya wengi. Hapa kuna haja ya kukuza na kudumisha vipaji nakarama za vijana katika ulimwengu wa kazi, ili hatimaye, kuwa na vijanawanaoshiriki kikamilifu katika kudumisha mshikamano wa dhati na jirani zao. Leohii changamoto kubwa ni mchakato wa utandawazi wa teknolojia, dhana inayopaswakujikita katika mshikamano, ustawi na maendeleo ya wengi.
Vijana wapewe nafasi ya kushiriki katika ugunduzi utakaosaidia kuendelezasekta mbali mbali za uzalishaji na huduma kwa jamii. Serikali, Makampuni nawatu binafsi wanapaswa kuonesha mshikamano, ili kusaidia kusongesha mbelegurudumu la maendeleo na ustawi wa wengi. Kama Halmashauri ya Wilaya yaSumbawanga tuna wajibu wa kulinda utu, wajibu na heshima ya kazi mahali pa kazi pamoja na kushiriki maadhimisho hayo kwa kila mwaka.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa