• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

Kilimo

Mazao yanayolimwa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ni mahindi, mpunga, maharage, mtama, ulezi, karanga, mihogo, alizeti, mtama, ngano, mbaazi, kunde na ufuta.

Idara ya Kilimo katika Halmashauri ina majukumu yafuatayo :

  • Kukuza na kusimamia shughuli zote za kilimo katika halmashauri
  • Kutoa huduma za ugani kwa wakulima kwa kushirikiana na wadau wengine.
  • Kuhakikisha Jamii inajitegemea kwa chakula
  • Kuboresha na kudumisha miundombinu ya kiuchumi kwa kuweka mkazo katika ujenzi wa maghala, miundombinu ya masoko na miradi ya umwagiliaji.
  • Kuwezesha na kuendeleza vyama vya akiba mikopo (SACCOS) katika ngazi ya kata kama njia pekee kuelekea ukuzaji wa mitaji ya fedha vijijini.

Dira,Mwelekeo na Malengo ya Idara:

Dira

Kujenga idara ya kilimo yenye tija, faida, ambayo hutumia maliasili katika ujumla, katika hali endelevu katika Halmashauri kufikia mwaka 2025.

Mwelekeo:

Kuwezesha mabadiliko ya kisasa ya sekta ya kilimo katika Halmashauri , biashara ya ushindani, usalama wa chakula na kupunguza umaskini kwa njia ya kuongeza tija na uzalishaji wa bidhaa za mazao.

Lengo Kuu.

Kuendeleza ufanisi, ushindani na faida ya secta ya kilimo ambacho kinachangia uboreshaji wa maisha ya watu katika Halmashauri na kufikia ukuaji mkubwa wa kiuchumi na kupunguza umasikini

Malengo Maalumu.

  • Kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza miundo mbinu ya kiufundi ( zana za kilimo, umwagiliaji, ugani na mafunzo).
  • Kuongeza uzalishaji, tija na faida kutokana na matumizi ya rasilimali za uzalishaji - Ardhi Nguvukazi Mtaji na muda.
  • Kuongeza chakula,kuboresha lishe na uzalishaji wa chakula cha ziada.
  • Kuboresha usindikaji wa mazao ya kilimo kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuongeza ajira.
  • Kuboresha uzalishaji wa bidhaa bora ili kuongeza ushindani wa bidhaa za kilimo katika masoko ya Halmashauri, , Mikoa ,kitaifa na kimataifa
  • Kutoa mazingira mazuri ya kuvutia sekta binafsi katika uwekezaji katika Halmashauri kweye eneo la usindikaji wa mazao ya kilimo.
  • Kuimarisha ushirikiano baina ya sekta ya kilimo na wadau wengine ili kuongeza ufanisi
  • Kulinda na kuendeleza matumizi endelevu ya ardhi ya kilimo.
  • Kukuza utekelezaji wa masuala mtambuka katika kutekeleza shughuli za kilimo katika Halmashauri.

 Ufipa ya juu

  • Ukanda huu unachukua asilmia 70% ya jumla ya eneo la Halmashauri.
  • Ukanda huu unapatikana mita 1,700 juu ya usawa wa bahari
  • Ukanda huu upo kati ya mabawa mawili ya bonde la ufa.
  • Katika maumbile, ukanda huu kwa sehemu kubwa ni nyasi.
  • Ni eneo la kilimo ambalo uzalishaji wa mazao hutoa ziada kubwa.
  • Mazao yanayozalishwa katika eneo hili ni mahindi, maharage, alizeti, mtama , karanga, miwa na aina za mbogamboga.

 Bondela Ziwa Rukwa 

  • Ukanda huu unachukua asilimia 30% ya jumla ya eneo la Halmashauri .
  • Mwinuko wake ni hadi mita 810 juu ya usawa wa bahari .
  • Eneo hili lipo kati ya bonde la Lyambalyamfipa na Ziwa Rukwa.
  • Eneo hili linaonekana kuwa matumizi yake yapo chini ya kiwango katika uzalishaji wa mazao mbalimbali kulingana na uwezo wa eneo, lakini kuna idadi ya mifugo inayozidi maeneo ya malisho.
  • Asilmia 85% yamifugo (Ng'ombe)katika Halmashauri ya Wilaya ipo katika eneo hili.
  • Ukanda huu ni mzuri kwa ajili ya uzalishaji wa mpunga, mtama na aina mbalimbali ya miti ya matunda.
  • Eneo hili pia likokatika mazingira yanayofaa kwa uzalishaji wa mazao yanayotoa mbegu za mafuta kama vile; migazi ,minazi, alizeti, ufuta na karanga,

VITENGO VYA IDARA YA KILIMO

Vifuatavyo ni vitengovya idara na majukumu yake

Kitengo cha Mazao .

  • Kuendesha mafunzo kwa wataalam wa Kilimo,
  • Kufanya ufuatiliaji juu ya mwenendo wa masoko ya bidhaa za mazao ya kilimo .
  • Maandalizi ya mipango na taarifa ya utekelezaji wa sekta ya Kilimo,
  • Kupanga na kufanya Maandalizi ya kusambaza mbegu bora,
  • Kushiriki katika utafiti wa mbegu mpya iliyoanzishwa kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kibali kwa ajili ya matumizi.
  • Kupanda na kusimamia mbegu za msingi zilizotolewa na watafiti,
  • Kusimamia mashamba ya majaribio ya mbegu na maabara ya majaribio ili kuangalia ubora wa mbegu hizo.
  • Kuhamasisha kuhusu uzalishaji wa mazao mapya yaliyoanzishwa.
  • Kuandaa mipango na bajeti ya sekta ya Kilimo katika ngazi ya Halmashauri.
  • Kuanzisha sera na sheria ndogo ndogo zinazoongoza uanzishwaji wa mazao na uzalishaji.
  • Kuandika taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kilimo.

 Kitego cha huduma za ugani.

  • Kuwafahamisha wadau kuhusu teknolojia mpya iliyoanzishwa.
  • Kuhamasisha juu ya uanzishwaji na malezi ya vikundi vya wakulima.
  • Kuhamasisha uzalishaji wa mazao mapya yaliyoletwa katika Halmashauri
  • Kuhamasisha na kusimamia uwekezaji wa Kilimo katika Halmashauri
  • Kuendesha mafunzo kwa wauzaji pembejeo za kilimo
  • Kuandaa, kutunza na kutoa takwimu na kumbukumbu za mahitaji, matumizi , hisa na bei ya pembejeo za kilimo kwa wauzaji na wawekezaji.
  • Kuandaa na kupitia upya ramani za vijiji
  • Kusimamia mitandao ya mawasiliano ya Kilimo katika Halmashauri
  • Kupanga na kusimamia shughuli zote za ugani katika Halmashauri na kutoataarifa ya utekelezaji
  • Kushirikiana na mashirika yasiyo ya Serikali katika kuanzisha vikundi vya wakulima katika uzalishaji, usindikaji na masoko ya bidhaa za Maua (Matunda, viungo, maua na mbegu)
  • Kushirikiana na watafiti katika uanzishwaji wa mashamba ya kilimo majaribio
  • Kuanisha maeneo ya uwekezaji ya Kilimo katika Halmashauri
  • Kuratibu manunuzi, uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo katika ngazi ya Halmashauri.

Kitengo cha lishe

  • Kuandaa taarifa ya hali ya chakula katika Halmashauri
  • Kuendesha mafunzo juu ya lishe ya binadamu na kuanndaa bajeti ya chakula katika kaya
  • Kutoa mafunzo juu ya usindikaji na utunzaji chakula katika ngazi ya Kaya
  • Kufanya ufuatiliaji juu ya usalama wa chakula na masoko ya masoko ya chakula

 Kitengo cha mazao ya bustani

  • Kuanzisha na kusimamia kilimo mazao ya bustani , usindikaji na masoko ya mazao ya bustani
  • Kuanzisha na kusimamia uzalishaji wa mbegu bora za maua
  • Kufanya mafunzo juu ya kilimo cha bustani na usindikaji wa bidhaa zitokanazo na mazao ya bustani
  • Kuhamasisha uanzishaji wa kilimo cha bustani

Kitengo cha Umwagiliaji 

  • Kufanya utafiti wa mazao ilikujua ni mazao yapi yanafaa katika maeneo ya Umwagiliaji.
  • Kuanzisha na kuratibu mipango na mikakati ya kudumu ya kilimo chaUmwagiliaji.
  • Kuandaa mapendekezo kwa ajili ya uboreshaji wa kilimo cha Umwagiliaji wa asili.
  • Ukusanyaji na utunzaji wa takwimu na kumbukumbu zinazohusiana na kilimo chaUmwagiliaji .
  • Kushirikiana na wadau mbalimbali katika ujenzi wa miradi /scheme za umwagiliaji mashambani.
  • Kushirikiana katika utafiti kwa ajili ya maeneo yanayofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji.
  • Kushirikiana na wadau mbalimbali katika ujenzi wa mabwawa.
  • Kufanya mafunzo ya wakulima kuhusu uendeshaji wa miradi ya Umwagiliaji.

Kitengo cha Ardhi,udongo na Matumizi bora ya Ardhi. 

  • Kutoa mafunzo kwa wakulima juu ya uhifadhi wa udongo na maji mashambani.
  • Kufanya uchunguzi wa udongo.
  • Maandalizi ya sera na matumizi ya ardhi na kusimamia sheria ndogo ndogo.
  • Kusomaramani na kutafsiri.
  • Kukusanya na kuweka takwimu za udongo na kumbukumbu.
  • Kushirikiana katika kuanzisha mipango inayohusu matumizi bora ya ardhi na malisho ya mifugo
  • Kufanya tathmini ya athari za matumizi ya ardhi katika Halmashauri.

Kitengo cha zana za kilimo. 

  • Kufaya Maandalizi ya zana mbalimbali za kilimo, kutoa mafunzo ya vitendo na kutoa ushauri wa kiufundi juu ya matumizi na utunzaji sahihi wa zana za kilimo
  • Kukusanya na kuweka takwimu na kumbukumbu zinazohusiana na zana za kilimo.
  • Kuandaa na kutoa taarifa kuhusiana na zana za kilimo katika Halmashauri.
  • Kutoa ushauri katika matumizi sahihi ya zana za kilimo na njia sahihiza usafirishaji wa mazao katika maeneo ya mashambani.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 10, 2025
  • Baraza la Mitihani Tanzania latangaza matokeo ya darasa la saba 2024 October 29, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Tazama

Habari Mpya

  • Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

    September 05, 2024
  • Makabidhiano ya ofisi

    August 21, 2024
  • CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

    July 25, 2024
  • Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa

    May 25, 2024
  • Tazama

Video

Kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 0754634811

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa