• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Tarehe ya kuwekwa: December 16th, 2022

Waziri Mkuu Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa Amefanya ziara ya kikazi mkoani Rukwa na kutembelea wilaya zote tatu kwa mda wa siku tatu.

Akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Majaliwa Majaliwa aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa ofisi ya mkurugenzi inayojengwa katika mji mdogo wa Laela. Pia alipata wasaa wa kuongea na wananchi juu ya maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na DR. Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na hilo pia Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa  alisisitiza mawakala wa mbolea kusambaza mbolea sehem zote za Wilaya ya Sumbawanga ili wakulima waweze kunufaika na punguzo la bei ya mbolea maana huu ni msimu wa kilimo.

Pia Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa aliwasihi wananchi kutunza miradi yote inayojengwa  ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga hususani Madarasa, Hospitali na Miundombinu ya maji. Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alisisitiza pia upandaji wa miti na kuitunza ili kuendelea kutunza mazingira.

Pia swala la ukosefu wa maji katika mji mdogo wa Laela alisema serikali imesikia kilio cha wana Laela na kusema inalifanyia kazi ingawa tayali kuna mkandarasi anajenga tanki za maji ili kuweza kusafilisha maji toka mto kwela hadi Laela.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa hakusita kusifia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga unao ongozwa na Bi. Ligtness S Msemo Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa umahiri wa kusimamia miradi kwa uadilifu mkubwa.

Baada ya ziara hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alifanya mazungumzo na watumishi wa Mkoa wa Rukwa kwenye ukumbi wa St. Maurus. K atika mazungumzo hayo Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alisisitiza sehem zifuatazo.

Uadilifuna uaminifu  makazini ili kuweza kuwatumikia wananchi wote kwa usawa. Pia ili kuweza kusimamia miradi yote pasipo na mashaka.

Kujenga timu mahusianoazuri kazini Kwa ajili ya ushirikiano ili kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano mkubwa lengo ni kuwa na matokeo chanya katika Nyanja zote.

Pia aliongelea swala la wajasiliamali wadogo wadogo wafahamikao kwa jina la wamachinga lengo ni kila Halmashauri itenge eneo kwa ajili ya wafanyabiashara hao ili kuongeza ufanisi katika biashara zao.

Uwepo wa dawa kwenye vituo vyote vya huduma za afya, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alisisitiza dawa ziwe zinanunuliwa kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma pasipo shaka. Pia juu ya hilo alisema wahudumu wa afya wote wawe waadilifu na kuzitunza dawa hizo na sio kufanya vinginevyo.

Kuwa na vikao mala Kwa mala kati ya wafanyakazi kwa wafanyakazi na wafanyakazi na wanachi ili kukumbushana majukumu yetu ya kila siku pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi walau siku tatu kwa wiki.

Kuendelea kubaini vyanzo vipya vya mapato Kwa ajili ya kukusanya mapato Ili kuweza kukidhi matumizi ya Halmashauri. Kuendelea kutumia mashine (POS) Kwa ajili ya kukusanyia mapato na kuepuka kutumia pesa mbichi.

Pesa zinazotoka Serikali kuu zifanye kazi elekezwa Kwa ufanisi Ili kuweza kunufaisha Wananchi na sio kubadilisha matumizi au kuanzisha miradi bila kukamilisha.

Kutambua mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya Taifa.

Kuimarisha sekta ambazo zinamahitaji makubwa Kwa Wananchi hususan Hospitali na Shule. Pia kuweka mazingira sahihi ya elimu ili watoto kuanzia miaka 4 waweze kuanza darasa la kwanza wakiwa wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu.

Ruwasa ihakikishe Kila Kijiji kinapata maji Ili kutimiza adhima ya mama Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Barabara ziweze kupitika Ili kurahisisha mawasiliano ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili pia iweze kusaidia katika kuingua uchumi wa nchi yetu.

Aliagiza Afisa ugani na mifugo kutatua matatizo ya migogoro ya Aridhi ili kupunguza au kuondoa mikwaruzano isiyo ya lazima baina ya wakulima na wafugaji.

Kila wilaya ijitajidi kuvumbua vyanzo vya kitalii ili kuvutia watalii na kuongeza sehem za utalii Ili kuvutia watalii lengo kubwa ni kuongeza mapato ya Halmashauri.

Upande wa Maslahi ya watumishi, Serikali imefanya kazi kubwa kupunguza madeni na kuendelea kupandisha madaraja watumishi. Na hili zoezi niendelevu hivyo serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan itahakikisha kila mtumishi wa uma anafikiwa na neema hiyo.

Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alimaiza kwa kuwashukuru watumishi wote waliojitokeza na kufunga kikao.

Matangazo

  • Baraza la Mitihani Tanzania latangaza matokeo ya darasa la saba 2024 October 29, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Orodha ya asasi zilizopata kibali cha uangalizi wa uboreshaji wa daftari mwaka 2024/2025 June 26, 2024
  • Tazama

Habari Mpya

  • Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

    September 05, 2024
  • Makabidhiano ya ofisi

    August 21, 2024
  • CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

    July 25, 2024
  • Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa

    May 25, 2024
  • Tazama

Video

Kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 0754634811

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa