Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 4 zilizomo katika Mkoa wa Rukwa.Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ina kanda mbili ambazo ni ukanda wa Bonde la ziwa Rukwa na ukanda wa Ufipa ya juu ikiwa na jumla ya Kata 27 na Vijiji 114. Wastani asilimia 85 ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wanategemea shughuli za kilimo. Idadi ya watumishi waliopo sehemu ya kilimo ni 29 katika idadi hiyo watumishi waliopo makao makuu ni 4 na watumishi 25 wapo maeneo ya Kata na Vijiji, Mahitaji ya watumishi sehemu ya kilimo ni 27 hivyo upungufu ni watumishi 2 ngazi ya Kata.
Hali ya hewa
Kutokana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kuwa unyeshaji wa mvua msimu wa 2023/2024 utaanza wiki ya pili au ya tatu na utakuwa ni wa juu ya wastani hadi wastani wakulima tunashauriwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni pamoja na kuzingatia mabadiliko tabia nchi.
Pamoja na kuwepo kwa mvua hizo athari chanya na hasi zinaweza kujitokeza
Athari chanya
Athali hasi
Ushauri kwa wakulima
Wakulima wanashauriwa yafuatayo; Kutumia kanuni bora za kilimo na Kutumia mbinu bora na himilivu pamoja na teknolojia za kuzuia maji kutwama na kuzuia mmomonyoko wa udongo shambani pia Kuwasiliana kwa ukaribu na maafisa Ugani waliopo katika maeneo yao au jirani na maeneo yao.
Huduma za ugani
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga huduma za ugani zinatolewa kupitia maafisa Ugani waliopo makao makuu , Kata na Vijiji vilevile kwa kushirikiana na wadau wa kilimo katika kuanzisha mashamba darasa na mashamba ya mfano pia utoaji wa mafunzo/elimu kuhusu kanuni za kilimo bora.
Uzalishaji
Malengo ya uzalishaji kwa msimu wa 2022/2023 yalikuwa ni tani 495,917.44 katika eneo la ukubwa wa hekta 225,804.7 na uzalishaji ulikuwa tani 496,072.25 katika hekta 189,411.80.
Malengo ya uzalishaji kwa msimu 2023/2024 ni kuzalisha tani 595,544.70 katika eneo la ukubwa wa hekta 218,501. Ili kuhakikisha kwamba kuna ongezeko la uzalishaji tija kwa mazao yote Serikali kupitia Wizara ya kilimo imetoa kifaa cha kupimia afya ya udongo ambapo zoezi la uchukuaji wa sampuli za udongo kwenye mashamba ya wakulima limeanza kufanyika ili wakulima waweze kujua ni aina ipi na kwa kiasi gani cha mbolea kinahitajika kwa zao husika.
Utaratibu wa upatikanaji wa Pembejeo
Serikali kupitia Wizara ya kilimo inatoa pembejeo za kilimo hususani mbolea kwa njia ya ruzuku kupitia mawakala waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.Idadi ya mawakala waliokuwepo msimu 2022/2023 ni 6 na kwa msimu huu idadi ya mawakala imeongezeka hadi kufikia mawakala 16,idadi ya mawakala inaweza kuongezeka kutokana na wadau kuendelea kuomba uwakala wa mbolea za ruzuku . Jedwali hapo chini linaonesha majina ya mawakala waliopo mpaka sasa
S/NA.
|
JINA LA WAKALA
|
KITUO ALIPO
|
NAMBA YA USAJILI
|
1
|
BEDA MAJALIWA
|
LAELA
|
TFRA - 5567
|
2
|
WINFRIDA MAJALIWA
|
KASANZAMA
|
TFRA - 5570
|
3
|
FRED SIWONIKE
|
KASANZAMA
|
TFRA - 5576
|
4
|
BARAKA KAYOMBO
|
LAELA
|
TFRA -6926 -8067
|
5
|
MBALA AMCOS
|
LAELA
|
TFRA -6981 -7488
|
6
|
LAELA AMCOS
|
LAELA
|
TFRA -6981-7501
|
7
|
REGIUS KAFULUSU
|
LUSAKA
|
TFRA -7099-7176
|
8
|
RAPHAEL KAJELA
|
IKOZI
|
TFRA - 5575
|
9
|
QUEEN KIBONA
|
MPUI
|
TFRA - 5573
|
10
|
ELINEO CHAULA
|
MPUI
|
TFRA - 06 - 4877 - 6927
|
11
|
ROBERT KAYUWI (KALOLO AGRO VET)
|
MPUI
|
TFRA - 06 - 4877 - 8033
|
12
|
ABEL MSUMBACHIKA
|
MPWAPWA/KAENGESA
|
TFRA - 5082
|
13
|
NYERERE AMCOS
|
MUZE
|
TFRA-6981-8415
|
14
|
MANFRED BUGUBUGU
|
MTOWISA
|
TFRA-
|
15
|
VUMA AMCOS
|
MTOWISA
|
TFRA-6981-
|
|
|
|
|
|
|
|
|
16
|
SAMOLA AGROVET
|
ILEMBA
|
TFRA-7457
|
Usajili, uhuishaji na usambazaji wa mbolea kwa wakulima
Katika kutekeleza mpango wa utoaji mbolea za ruzuku msimu 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ilisajili wakulima 23,341 ambapo mahitaji ya mbolea kwa msimu huo yalikuwa ni tani 4,500 Idadi ya wakulima walionunua mbolea ilikuwa ni 9,713 sawa na asilimia 41.6 ya wakulima wote waliosajiliwa kwenye mfumo, kiasi cha Tani 6,601 kilinunuliwa na wakulima . Idadi ya wakulima waliosajiliwa Kwa msimu wa 2023/2024 ni 5,477 hivyo kufanya jumla ya wakulima 28,818 waliosajiliwa kwenye mfumo wa kidigitali kati ya wakulima 46,127, zoezi la usajili na uhuishaji wa taarifa za wakulima linaendelea na mpaka sasa wakulima waliohuishwa kwenye mfumo ni 6,716 kati ya 23,341 waliosajiliwa msimu uliopita.
Mahitaji ya mbolea kwa msimu huu ni tani 7,051, Kiasi kilichosambazwa ni tani 2,343 na kilichouzwa kwa wakulima ni tani 2,181 kiasi kilichopo ni tani 162. Mbolea za ruzuku zinauzwa kwa bei elekezi iliyotolewa na Serikali kuanzia mwezi Septemba ambazo zinaanzia Tsh. 77,805 hadi Tsh.78,812 kwa mbolea ya kupandia na kwa mbolea ya kukuzia ni Tsh. 67805 hadi Tsh.68,811 kwa mfuko wa kilo 50.
Usambazaji wa mbegu katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga unafanyika kupitia mawakala wa pembejeo za kilimo (Agro dealers). Kwa msimu wa 2022/2023 mahitaji ya mbegu za nafaka,mikunde na mazao ya mafuta ni tani 688 na kiasi cha mbegu kilichotumika ni tani 775. Mahitaji ya mbegu kwa msimu 2023/2024 ni tani 1,305.
Changamoto
Mgeni rasmi pamoja na maelezo hapo juu Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ina kabiliwa na changamoto zifuatazo;
Utatuzi
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa