Mwenge wa Uhuru umekimbizwa wilaya ya Sumbawanga tarehe 20/9/2021 na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 10 ambayo ni Elimu 2, Maliasili 1, TEHAMA 1, Utoaji Mikopo 2, Afya 2, Mradi wa Umeme 1 na Barabara 1. Thamani ya miradi yote ni shilingi 8,753,603,292/-, kati ya kiasi hicho Serikali kuu imetoa Shilingi 8,632,087,292/-, Wilaya imechangia Shilingi 104,466,000/-, Wananchi wamechangia Shilingi 2,250,000/- na Wadau wengine wa Maendeleo Shilingi 14,800,000/-.
Ujumbe wa Mwenge
Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2021 umebeba ujumbe Mkuu usemao’’TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji’’’. Ujumbe huu unalenga kuhimiza umuhimu wa matumizi ya TEHAMA kwa maendeleo ya Watu kwani, kwa sasa matumizi ya TEHAMA kwa Wananchi yameongezeka katika nyanja mbalimbali za Kijamii Kilimo na ufugaji, Viwanda, Biashara, Afya na Elimu. Ongezeko la matumizi haya ya TEHAMA yamesaidia kwa kiasi kikubwa ongezeko la Uchumi na Ustawi wa Jamii kwani imerahisisha shughuli zao za kila siku. Pamoja na mafanikio hayo ya TEHAMA Wilaya imeendelea kusisitiza juu ya Matumizi sahihi ya TEHAMA. Hivyo Wananchi wanawajibu wa kufuata kwa usahihi matumizi ya TEHAMA kwa kufuata kanuni, Sheria na Taratibu. Hivyo Wananchi wanawajibika kutambua matumizi sahihi ya TEHAMA ikiwa pamoja na utunzaji wa miundombinu yake.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa