Kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi tarehe 28/10/2021 katika ukumbi wa kituo cha kilimo Laela kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Ndg Kalolo Ntila, kimepokea na kujadili taarifa mbalimbali ikiwemo taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, kikao hicho ambacho ni cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2021
Upande wa mapato hadi kufikia Septemba 2021, Halmashauri imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS 2,345,153,600.00 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali.
Kati ya fedha hizo makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani ni kiasi cha TZS 370,808,391.11 sawa na asilimia 13, Ruzuku ya Mishahara ni TZS 1,667,479,000.00 sawa na asilimia 7, Mapato mengineyo ni TZS 34,071,500.00 sawa na asilimia 2 na Fedha za Miradi ya Maendeleo ni kiasi cha TZS 272,794,709.00 sawa na asilimia 3.
Makusanyo hayo ya Mwezi Septemba 2021 yamepelekea kuwa na jumla ya ya kiasi cha TZS 6,751,698,717.00 kwa kipindi cha Julai –Septemba 2021 sawa na asilimia 17 kwa mchanganuo ufuatao;-
Pia iliwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hadi kufikia tarehe 30 Juni 2021, Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 950,313,489/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo saw ana asilimia 7.6 ya fedha ya miradi.
Kati ya fedha hizo, 567,563,383/= ni mapokezi ya fedha nje ya ukomo wa bajeti saw ana asilimia 59.4 ya mapokezi ya fedha za miradi. Halmashauri imetumia jumla ya shilingi 239,801,600.2 sawa na asilimia 42.25 ya mapokezi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Sebastian Waryuba, aidha alitoa maelekezo kwa taasisi za Serikali kama TARURA na nyinginezo kuwa “wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni mafuruku kuwa na bajeti ya dharura (emergency budget) kwa sababu zinaongeza gharama za miradi na kusababisha miradi hiyo kutokukamilika kutokana na kuisha kwa fedha, hivyo ni lazima kuongeza umakini wakati wa uandaaji wa gharama za miradi” aliongeza kuwa mabadiliko ya gharama yafanyike tu pale ambapo kuna ulazima wa kufanya hivyo mfano barabara imepitiwa na mkondo wa maji.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa