Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi 28,847,443,909.99 kutoka katika vyanzo mbalimbali kati ya TZS 33,073,542,339 ya lengo la mwaka, hayo yamesemwa leo tarehe 21/8/2021 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ndg. Gerald Kalolo Ntila katika kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi katika ukumbi wa chuo cha kilimo kilichopo katika Mamlaka ya Mji mdogo Laela ambapo ndio makao Makuu ya Halmashauri hiyo.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri amefafanua kuwa, mapato hayo yametokanana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani TZS 2,381,429,474.77, mishahara TZS 19,040,971,530, mapato mengineyo 1,059,055,127.89 na mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni TZS 6,365,987,776.
Mheshimiwa Mwenyekiti aliendelea kufafanua kuwa pesa hiyo imetumika katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi ya maendeleo TZS 5,206,276,728, mishahara 19,044,192,530, matumizi ya mapato ya ndani 2,028,445,814 na matumizi mengineyo 1,003,858,622.
Mh. Mwenyekiti alihitimisha kwa kutoa wito kwa watumishi wote kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuongeza nguvu kwenye suala la kukusanya mapato na kusimamia miradi ya maendeleo kwa uadilifu ili kuleta tija ya fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo.
SUMBAWANGA
Anwani ya Posta: P.O.BOX 229
Simu ya Mezani: 025-2802133
Simu ya Kinganjani: 0754634811
Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz
Hati MilikiĀ©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa