• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Sumbawanga District Council
Sumbawanga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji, Uthibiti wa Maji Taka
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • Ufungaji wa Nyuki
      • Tehama
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Shughuli za Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya fedha utawala na mipango
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Huduma za jamii(Elimu, Afya na Maji)
      • Kamati ya ujenzi uchumi na mazingira
      • Kamati ya madili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Ratiba ya Mwenyekiti kuwepo Ofisini
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habrari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha

Halmashauri yafanya kikao cha kwanza cha baraza la madiwani katika makao makuu mapya.

Tarehe ya kuwekwa: November 22nd, 2019

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mara ya kwanza imefanya kikao cha baraza lake la madiwani kwenye makao makuu mapya yaliyopo katika Mamlaka ya mji mdogo Laela. Kikao hicho kilifanyika siku ya Alhamisi tarehe 21/11/2019 katika ukumbi wa Chuo cha Kilimo Laela.

Akiongea katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake alioutoa wa kuhamishia makao makuu ya Halmashauri kutoka Manispaa ya Sumbawanga na kuyapeleka kwenye mamlaka ya mji Mdogo wa Laela. Alisema dhamira ya Mh. Rais ni kuhakikisha huduma zinasogezwa kwa wananchi na haipaswi makao makuu ya Halmashauri mbili kuwa ndani ya Halmashauri moja.

Pia alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ndugu Nyangi John Msemakweli kwa kutekeleza agizo la Mh. Rais la kuahamia katika makao makuu mapya ndani ya siku 14 kama alivyo ahidi mbele ya Mh. Rais. Alisema jambo hilo lilikuwa ni gumu sana lakini Mkurugenzi amehakikisha jambo hilo limetekelezwa kama alivyoagizwa. Vile vile aliwapongeza watumishi ambao wamekwenda kuanza makazi mapya kwa kipindi cha muda mfupi bila kuathiri utendeaji wao wa kazi.

Pamoja na mambo mengine pia Mh. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri alizungumzia suala la baadhi ya Kata kuwa ziko umbali mrefu zaidi ya kilometa 150 kutoka  makao makuu ya Halmashauri hiyo. alitaja kata hizo ambazo ni Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui, na Mtowisa. Alisema kuna kila sababu ya kutazama ni kwa namna gani wananchi wa maeneo hayo wanaweza kusaidiwa kupata huduma kwa ukaribu.

Baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Wah. Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa kuweza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 6, Oktoba 2019 alipokuwa katika ziara yake ya siku 3 ndani ya Mkoa wa Rukwa ambapo aliiagiza halmashauri hiyo kuhamia Laela.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 10, 2025
  • Baraza la Mitihani Tanzania latangaza matokeo ya darasa la saba 2024 October 29, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Matokeo Ya Kidato Cha Sita Na Ualimu Ngazi Ya Cheti Na Diploma 2024 Yametangazwa July 13, 2024
  • Tazama

Habari Mpya

  • Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

    September 05, 2024
  • Makabidhiano ya ofisi

    August 21, 2024
  • CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

    July 25, 2024
  • Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa

    May 25, 2024
  • Tazama

Video

Kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

Potifolio Yetu

  • Wizara ya Tamisemi
  • Wizara ya Utumishi
  • Wizara ya Kilimo
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana Nasi

    SUMBAWANGA

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 229

    Simu ya Mezani: 025-2802133

    Simu ya Kinganjani: 0754634811

    Barua pepe: ded@sumbawangadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Hati Miliki©2017. Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Haki zote zimehifadhiwa